Muziekvideo
Muziekvideo
Credits
PERFORMING ARTISTS
Ibraah
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Ibrahim Abdallah Nampunga
Composer
Songteksten
Haukutaka kulea, wakati unalelewa, lazima uvunjie watu wazima heshima
Punguza mazoea unajifanya una-care, wakati umemtelekeza Fahima
Achana na walokutangulia wakati kesho yako hujui itakwangukia
Unaweza Wasafi ukatimuliwa, na Konde Gang ukaja kusign-iwa
Unashindana na mwanajeshi ambaye vita aliianza baba yako (Na hawezi)
Msalimie kipa la ndezi, mwambie hata akikesha kwa sango (Hatuhami Mbezi)
Nyimbo kaimbiwa Kajala, karauka na kupwita-pwita, acha papara
Naskia unachimba mikwara, hauna chochote wewe buma chakula
Mapenzi ya Konde na Kajala yanakuhusu nini kaka wee (Hayakuhusu)
Hata wakiongea video call na Paula lakini si mwanae (Hayakuhusu)
We njoo ukomae na muziki (Hayakuhusu), ona kina Chinga tunahit (Hayakuhusu)
Tumeanza jana hatushikiki (Hayakuhusu), umeona Sound from Africa haisikiki, imebuma wee
Mambo ya kuhonga waandishi wa habari nyi mmezoea, tunawajua
Hata Youtube zetu mnapochokonoa, si tunawajua, tunawajua
Kama vipaji mnavyo, sa wivu wa nini? Tufanye kazi na tusonge mbele
Kama vipaji mnavyo, na mnajiamini, ya nini sasa kupiga kelele
Akina Lokole si wanawapost, sababu ndio machawa wao, ndio machawa wao
Kila siku anawapromote, leo asikose ladha, ooh ladha ooh
Chondelei mrudie Fahima ukamtunze mwanao, yasiwe ya Mzee Abdul na Nasibu
Kumbuka kujinyima usimsahau mwanao, baadae akutunze usije pata aibu
Mapenzi ya Konde na Kajala yanakuhusu nini kaka wee (Hayakuhusu)
Hata wakiongea video call na Paula lakini si mwanae (Hayakuhusu)
We njoo ukomae na muziki (Hayakuhusu), ona kina Chinga tunahiti (Hayakuhusu)
Tumeanza jana hatushikiki (Hayakuhusu), umeona Sound from Africa haisikiki, imebuma wee
Written by: Ibrahim Abdallah Nampunga


