Featured In

Lyrics

[Verse 1]
Farao kasimama mbele ya Musa
Akamuuliza Musa huyo Mungu wenyu ni nani
Farao akamwambia Musa
We Musa Mungu wenyu mimi simujui
[Verse 2]
Moyo wa Farao ulikuwa mgumu sana
Kumuelewa Mungu, Mungu wa Mbinguni
Moyo wa Farao ulikuwa mgumu sana
Kumuamini Mungu, Mungu wa Mbinguni
[Verse 3]
Mungu kampiga Farao kwa mapigo kumi
Ili Farao amjue Mungu
Mungu kampiga Farao kwa mapigo kumi
Ili Farao amjue Mungu
[Verse 4]
Pigo la kwanza maji yakawa Damu
Pigo la pili vyura mji mzima
Pigo la tatu Vumbi ikawa chawa
Pigo la nnenzi mji mzima
Pigo la tano magonjwa kwa wanyama wote
Farao amjue Mungu
[Verse 5]
Pigo la sita majipu kwa watu wote
Pigo la saba radi na mvua ya mawe
Pigo la nane nzige mji mzima
Pigo la tisa giza kwa siku tatu
Pigo la kumi wazaliwa wa kwanza wakafa
Mpaka wale, wale wa Farao
[Verse 6]
Hapo najifunza kumbe Mungu
Anapigana na adui zetu mama
Hapo najifunza kumbe Mungu
Anapigana na watesi wetu
[Chorus]
Oh adui zako (Watapigwa na Mungu)
Hao adui zako mama (Watapigwa na Mungu)
Wanaokupangia mabaya we (Watapigwa na Mungu)
Wanaokuendea kwa waganga (Watapigwa na Mungu)
Waliokupiga vita wewe (Watapigwa na Mungu)
Waliosema laana juu yako (Watapigwa na Mungu)
Oh watapigwa na Mungu (Watapigwa na Mungu)
Oh watapigwa na mungu (Watapigwa na Mungu)
[Verse 7]
Mungu nafanya vitu
Mungu nafanya vitu oh
Wako watu wanapigana nawe ndugu yangu
Usihangaike nao
Wako watu wanapigana nawe mama yangu
Usihangaike nao
[Verse 8]
Wako watu wanaokuendea kwa waganga
Usihangaike nao
Wamesema maneno ya laana juu yako we mama yangu
Usihangaike nao
Mwambie Mungu apigane nao
Mwambie Mungu apigane nao
[Verse 9]
Goliathi aliwatukana wana wa Israeli pamoja na Mungu wao
Goliathi aliwatukana wana wa Israeli pamoja na Mungu wao
Ghadabu ya Mungu ikashuka ndani ya Daudi
Ghadabu ya Mungu ikawaka ndani ya Daudi
[Verse 10]
Mawe matano laini yalitosha kabisa kumpiga Goliathi
Mawe matano laini yalitosha kabisa kumpiga Goliathi
Walio kinyume na wewe mama yangu watapigwa na Mungu
Wanaokuwazia mabaya watapigwa na Mungu
Wanao kusema vibaya watapigwa na Mungu
Watapigwa na Mungu
[Chorus]
Oh adui zako (Watapigwa na Mungu)
Hao adui zako mama (Watapigwa na Mungu)
Wanaokupangia mabaya (Watapigwa na Mungu)
Wanaokuendea kwa waganga (Watapigwa na Mungu)
Waliokupiga vita wewe (Watapigwa na Mungu)
Waliosema laana juu yako (Watapigwa na Mungu)
Oh watapigwa na Mungu (Watapigwa na Mungu)
Oh watapigwa na mungu (Watapigwa na Mungu)
[Verse 11]
Atakayekulaani atapigwa na Mungu
Atakayekulaani atapigwa na Mungu
Atakayekubariki atabararikiwa tu
Atakayekubariki atabararikiwa tu
[Verse 12]
Maana Mungu ni adui wa maadui zetu
Maana Mungu ni mtesi wa watesi wetu
Maana Mungu ni adui wa maadui zetu
Maana Mungu ni mtesi wa watesi wetu
Yeye ni Mungu ni Mungu mwenye nguvu nyingi
Yeye ni Mungu hashindwi na lolote
[Chorus]
Oh adui zako (Watapigwa na Mungu)
Hao adui zako mama (Watapigwa na Mungu)
Wanaokupangia mabaya (Watapigwa na Mungu)
Wanaokuendea kwa waganga (Watapigwa na Mungu)
Waliokupiga vita wewe (Watapigwa na Mungu)
Waliosema laana juu yako (Watapigwa na Mungu)
Oh watapigwa na mungu (Watapigwa na Mungu)
Oh watapigwa na mungu (Watapigwa na Mungu)
Written by: Christopher Mwahangila
instagramSharePathic_arrow_out