Lyrics
Kumbe simu ushaipokea mama naomba basi tuongee
Maana mwanao mi nina machungu saana,Naomba unisikie
Kweli najua hali yetu ngumu saana lakini usilie
Huku mjini mwanao mi napambana,Kidogo nikuletee
Uzuri mama ulinifunza kazi ngumu
Na nikayajua majukumu
Nikikosa sipaswi kulaumu
Mungu ndiye mwenye wakati muhimu mama
Kazi yangu naokota makopo
Ofsi yangu jalala nikipata chakula ni ukoko
Na mikate ya jalala
Mama kweli namiss huko ila kuja ni msala
Natafuta japo vimaokoto nyumbani nirudi na hela
Mama nisikudanganye mie hukuniliko,Nateseka asee
Nashindwa hata nifanyaje kwa maisha yako yanaumiza asee
Ila ngoja nipambane mi mtoto wako ndo ushakua mzee
Namiss utani wako sipo kalibu yako nabaki lia mie
Ooooh mama, ooooh ooooh mama
Written by: Omari Bakari Chalumoso


