Lyrics

Siku za mwisho za baba kitandani akiwa sick Leila yupo chumba cha mtihani wa form six Akinipigia simu ananiuliza how is he? Napata hisia mbaya kaka sipati usingizi Na nikilala ninamouta sana baba siku hizi Kaka naomba niambie ukweli please! Namjibu dad anaendelea vizuri na yuko nyumbani I hope utafanya vizuri kwenye mitihani I promise you my brother, lazima niende college Ila kama upo na baba basi naomba nimpe pole Mh namwambia sahivi amepumzika Hata simu yake tu haruhusiwi kuishika Si unajua tena mzee anaumwa presha Docta kasema tumpe muda he will get better Maskini Leila, I wish nimwambie ukweli Ila sitaki kumchanganya ana mtihani asije feli Caz dad is gone, dad is not home Ndugu wanasema nimwambie walimu wanasema no Mama alikuwa analia sana ilibidi mi nijikaze Nikamwambia Leila, baba yuko poa usiwaze Na baba kama unaniskia nina Habari njema I wish hata ungesubiria matokeo ya Leila Leila amefaulu, division one, Nishamlipia school fees chuo kikuu mlimani Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu (This is not based on true story) Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu (I insist this is not based on true story) Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu Siku za mwisho za baba kitandani anaugua Salmaa, hana anachojua Mpaka baba Mungu anamchukua Salmaa, hana anachojua Mpaka leo miezi imesogea, bado Salmaa hakuna anachoelewa Sababu Salmaa ndio kwanza ana mwaka mmoja' Kwanini baba umeondoka haraka si ungengoja Offcourse akikua atapewa stori na ndugu Lakini I feel sorry hatokuwa na kumbukumbu Dah, hatomjua baba natamani kama kungekuwa na namba Akikua labda angekutafuta akakupiga akakupata I wonder, Maisha yake ya ukiwa bila baba Umemuacha akiwa anavaa pampers I guess ndivyo alivyoandikiwa, labda Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu (Hii wala sio true story) Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu (Narudia, hii wala sio true stori, ila nitaawambia hii ni nini) Dady umelala, but I remember you everyday uuu huu Siku za mwisho za baba kitandani akiwa hoi, sorry Siwezi kuendelea na stori Dada angu Neema anateseka sana siko sawa Mungu baba nyoosha mkono wako I believe your power Hii wala sio story ila nitawambia hii ni nini
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out