制作

出演艺人
Xouh
Xouh
表演者
作曲和作词
Ramadhan Daniel
Ramadhan Daniel
词曲作者

歌词

Nikianguka nitasimama
Mungu wangu anaona navyopambana
Kuniangusha ni ngumu sana
Namuamini Mungu
Naamini nachofanya
We mwenyewe si unaona navyopambana
Kuniangusha ni ngumu sana
Namuamini Mungu (Yah!)
Nimetumwa kusaka shilingi (Eeeh)
Nimetumwa na mdingi (Eeeh)
Nimetumwa na bimkubwa
Nimetumwa na babu na bibi
Nimetumwa na kijiji kizisaka shilingi
Nimetumwa na mtaa
Nikipatacho nashukuru
Nikikosa siwezi laumu
Kidogo changa chanistiri
Alhamdulillah (Amen)
Matatizo yangu namuachia Mungu
Hata nikiumwa ye ndo mtabibu
Yeye ndo anafanya nisipate taabu
Oohh!
Nikianguka nitasimama
Mungu wangu anaona navyopambana
Kuniangusha ni ngumu sana
Namuamini Mungu (Nyani zee eh!)
Naamini nachofanya
We mwenyewe si unaona navyopambana
Kuniangusha ni ngumu sana
Namuamini Mungu
Aah aah!
Kila njia nayopita ni salama
Nimelindwa na baraka ya Mungu pia ya mama
Nawekea gear naongeza gear zinafatana
Ni makeke na vurugu kwa mastyle ya kuchana
Poleni wanga mlijaribu ila amkubana
Mungu kanipa mwanga nashine mpaka ile laana
Nikikosa najipanga sio kwa mganga Mungu kwanza
Nalindwa na Mungu baba yaarabi toba siendi chaka
Nikidondoka nanyanyuka ananinyanyua
Nikipata kiu Mungu wangu analeta mvua
Amenifanya superstar kila kona wananijua
Kila chaka nakamua kwenye bar kwenye tour
Kila hatua dua Mipango ni ya Mungu
Binadam huwezi pangua
We kazi yako majungu mwanaharam tunakujua
Roho yako mbaya inakutu unakuja
Ungekujua haya yote ungeyajua
Ungekua ushatusua
Nikianguka nitasimama
Mungu wangu anaona navyopambana
Kuniangusha ni ngumu sana
Namuamini Mungu
Naamini nachofanya
We mwenyewe si unaona navyopambana
Kuniangusha ni ngumu sana
Namuamini Mungu
Written by: Ramadhan Daniel
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...