制作

歌词

Ni asubuhi ninaamka ninapiga mswaki
Kisha naenda ku-bath kuweka mwili safi
Narudi ghetto nafungua kabati
Nachukua pamba bling bling kwa chati
Nna t-shirt black nna jeanz ya kaki
Na chini nina simple white chata nike
Kisha mzee najipulizia marashi
Nanukia safi
Niko na machizi wa chamber squad na Dark
Tunawapigia simu Rich Coast wako wapi
Tunakutana mitaa ya Chaga Bite
Asubuhi tunapata zetu supu kwa chapati
Na mitungi ya kupotezea wakati
Ukitaka fegi mi zangu nna pakti
Iwe sports yani sm au embassy
Hapa utakula raha mpaka mwenyewe utasema basi
Tunakamua mpaka ile mida ya lunch
Tunaagiza ugali mkubwa na samaki
Makamuzi yanaendelea mpaka night
Watu wanaingia graveyard kwanza kupata nyasi
Tunarudi kila mmoja anajisachi
Ni kiasi gani mfukoni kilichobaki
Kujicheki mi nna kama laki
Nikawaambia machizi kinachofuata mikasi
Mitungi,blunt mikasi (oooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
Mitungi,blunt mikasi (oooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
Kulewa tushalewa kilichobaki mikasi
Washikaji eh milupo tutapata wapi?
Milupo labda mitaa ya kati
so tunaenda vipi kwa miguu au kwa bus?
Usiku huu bora tuchukue tax
Poa basi tusipoteze wakati
Psss psss naita tax
Njoo utupeleke mitaa ya kati
Tukacheki midudu ya kupiga mikasi
Tuelewane kabisa itatu-cost sh’ngapi?
Buku nne tu
Aah wapi
Kwani hapa na pale ni umabali wa hatua ngapi?
Si unacheki mwenyewe mko wangapi?
Usi-mind sana babake hatuko safi
Tuchangeni tusipoteze wakati
Ludigo kwani we una Tshs ngapi?
buku tano
Venture?
bati
sasa we unabati usiku huu unaenda wapi?
Wakati hiyo bati hata soda tu hupati
Bora uweke kesho unywee chai na chapati
Asiye na kitu mi naona bora akabaki
Tusije mbele tukashikana mashati
Suka eh! tuanzie Masaki
Mchizi kapiga simu yaani kuna bonge la party
Mitungi,blunt mikasi (oooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
Mitungi,blunt mikasi (oooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
Dereva funga break tushafika kwenye party
Eeeh bwana eh kumbe bonge la party
Cheki mademu kibao utadhani kitchen party
Duh! cheki lile anti lililovaa skin tight
Ee bwanaeh! Liko safi sio mchezo babake unaweza ukahonga laki
Aah wapi mtu kama mi hanipati
Usawa wenyewe huu wa kulenga kwa manati
Poa basi tujichanganye katikati
Tukacheki mitungi na mademu wa mikasi
Oya Braza mwenye black unaitwa na yule anti
Yuko wapi?
yule aliyevaa suti ya kaki
Anti vipi?
Aah safi samahani kwakukupotezea wakati
Nilikuwa naomba tuwe wote kwenye party
Au unasemaje?
Mi naona safi
Samahani wewe anti ambaye umevaa
Hivi unaitwa nani eh?
naitwa Bahati
Hivi anti nishawahi kukuona wapi?
Acha longolongo we sema una sh’ngapi
Oyaa we vipi mpangowako vipi?
Mbona mi mazee mpango wangu safi
Ishakuwa usiku twenzetu tukachukue tax
Twenzetu tukapige mikasi
Mitungi,blunt mikasi (oooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
Mitungi,blunt mikasi (oooh yeah)
Kama ukitaka kuvinjari nasi basi
Mfukoni mwako nawe uwe safi
Written by: Albert Keneth Mangwair (Ngwair), Feruzi Mrisho Rehani (Ferouz), Haji Ally Taikuni (Mchizi Mox), Ludigo Bishota (Professor Ludigo), Paul Peter Matthijsse (P-Funk Majani)
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...