Texty

(Lu-Lu-Lufa) Haueleweki hata uki-shine kwa punchlines on Facebook Haiwi-fine ka' Rayvan, we' fake tu Sikuoni B.E.T au MTV wak-play tunes Miaka nenda we' msanii, MC una play tu Makida, we' sio king kama Kiba Sio yao ming kwenye ring Mistari mingi zaidi ya zebra? (Zaidi ya zebra!) Unazingua nigga, haujajijua nigga Umeanguka pua, bishoo hauwezi kuwa Jigga Rent mwezi ujao na haujalipa school fees Ya mwanao, unaumiza kichwa ewe Q-Fid 'Til now hauioni future, we' stupid Haujapiga bao na kutwa unawaza groupies? Pengine ni nuksi umejiletea au chuki umejijengea Haukumbuki ulipotokea bro (bro) Wabaya mauzushi, wanayachochea haushtuki ushapotea Wakushi wanakutetea bro Unakosea bro, ni kweli hauna spear bro Ku-play fair, ikuwachezea ikatokea droo Sikutegemea bro, hatuwezi hataku'onea bro Tushajionea ulivyo mlevi, ukaikosea show Kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye) Kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye) Ayi, ma-mama, kiberiti Ayi, ma-mama Nikiwa alone in my room, sometimes I stare at the door And in the back of my mind, naziita hisia hebu njoo Zinaingia zinaniambia hii dunia ni soo Haiko sweet kama dove, I see, I need love Tazizo lako hautaki kuuza maneno Legeza ka' wenzako acha kutukuza misemo (kutukuza misemo) Sheria ni yako ila isiuache msumeno Ukijikuna tako, usikate kucha kwa meno Ongea usikike au kaa kimya usidharaulike Au utupishe na jina lisahaulike Tulazimike kuzima ili itulipe Gwajima tumuite aje kukupima heshima ya Bashite Nje ya town, show huwa zina cloud ya kiwaki Kaza crown ibaki, ukikaza sana hawataki Tunajua una uwezo wa juu na kismati Na haujawahi kupigwa bu! Basi unajiona Tupac Kabla ya rotten brothers ulikua na chepe Two nature boys ndiko ulikoanza makeke Mwaka huu, mwaka we mwaka Ikakuweka juu ikawa Q hakuna asiyemtaka, well Lini uta-retire urudi kuuza mtumba lango? Una roho mbaya, hadi leo haujamkumbuka Rado We' sio kichwa, we' unaweza fichwa Ikichorwa hip hop, siioni sura yako picha Kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye) Kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye) Ayi, ma-mama, kiberiti Ayi, ma-mama Fid Q nikuulize, hivi siri yako nini kuishi kwenye game muda mrefu, eh? Kwanza unajua, mi' huwa sichukulii vitu personal Ukiniponda sichukulii personal, ukinisifia sichukulii personal Ni'chojifunza ni kwamba usichukulie kila kitu personal Na zaidi, ufunze ubongo wako kung'amua jema kwenye situation yoyote ile Na hivi ndio vitu ambavyo Don Miguel kwenye kitabu chake cha The Four Agreements ameviongelea Kwa mfano, nikikutana na wewe sokoni au kokote na nikakuambia, "Wewe ni mjinga" Wakati hata sikujui, na siku hiyo hiyo ndio mara ya kwanza tumeonana Anaekua amevurunda hapo sio wewe ni mimi So kwa wewe kuchukulia personal na ku-react Ni sawa kuwa umekubaliana kihisia na jina hilo la mjinga Na huenda ukanifanya nijione mimi ni muoteaji mzuri Kuchukuria kitu personal ni kukubaliana moja kwa moja na kilichosemwa Na kama kweli umekubaliana inamaana kimekuingia Na kinapokuingia husambaza sumu ambayo huziua zile fikra chanya Ulizokuwa nazo na kufanya usichukue maamuzi sahihi Kila mtu anafanyanya vitu kwa ajili yake na kwa faida anazozijua yeye mwenyewe Ni mara chache sana wewe kuzing'amua hizo faida binafsi za watu Wengine utaona ni kwa ajili ya attention Wengine ni kwa sababu inawaingizia kipato Wengine iyo kitu huwaacha tu na furaha ya moyo Na vitu kadhaa wa kadha Kila mtu ana ndoto zake na pia hupendelea kufanya vile akili yake inamtuma Na pengine dunia tunayoishi sisi sio dunia wanayoishi wao Hivyo tunavyochukulia vitu personal ni sawa na kuwa- Kuwaaminisha ya kwamba tupo kama wanavyotufikikiria Na tunaota kuwa na utulivu kama walionao wakati sio kweli Na hata tusi liwe la nguoni kiasi gani Ni vyema ukajua na kuamini ya kwamba halikuhusu Kumbuka limjaalo mtu ndilo limtokalo Wengine wameathiliwa na malezi waliopitia pamoja na makuzi kwa ujumla So, hata mtu akiniambia we, yani Kwa mfano mtu akikwambia, "We Saida ni mshamba kuliko wasanii wote Tz" Ni vyema ukamsamehe tu! He! Lakini kumbuka kumsamehe mtu inamaana alikukwaza Uka-mind ndio maana ili usimfugie chuki na hasira Ndio maana inabidi umsamehe Na kumkasirikia inamaana uliruhusu ile sumu ikuingie Kwa hiyo kwenye hili mtu akikwambia, "Wewe ni mshamba kuliko wasanii wote" Tunashauriwa kumuacha kama alivyo tu Kwa sababu hizo ni hisia, imani na maoni yake yeye binafsi Na dawa pekee ya kuituliza iyo sumu Ni kuwapotezea tu ili waendelee kupambana na hali zao Watu wengi huwa wanashindwa kumjaji mtu kama alivyo Kutokana na vitu alivyonavyo Cha ajabu mentality hii imetupelekea sisi kuacha au kusahau kabisa Kuchukulia vitu kama vilivyo na kuanza kuvichukulia kama tulivyo Kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye) Kiberiti, ninakuona unavyoniwashia moto mie (aye) Ayi, ma-mama, kiberiti Ayi-yi, ma-mama Ninashangaa Kumbe wanadamu ndivyo walivyo Kumbe wanadamu ndivyo walivyo Ayi, ma-mama Ayi-yi, ma-mama Ninashangaa Kumbe wanadamu ndivyo walivyo Kumbe wanadamu ndivyo walivyo
Writer(s): Fareed Kubanda Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out