Songtexte

Ee Bwana nainamisha kichwa changu Ninakuabudu we Na tena nainua mikono yangu Kukuadhimisha we Na ninashuka kwa unyenyekevu Madhahabuni pako Maana majibu ya maswali yangu Baba nitapata kwako Kwanza nahitaji rehema zako Nisafishe Bwana Kwa yale nayajua na nisoyajua Niwe safi Bwana ninaomba neema yako Na kibali chako juu yangu wee Nitembee kifua mbele Yesu unapozuru wengine usinipite Nikumbuke, usinipite Maombi yangu, usinipite Baba uyakumbuke, usinipite Nyakati za majaribu, usinipite Niguse,usinipite Ingawa mi si mkamilifu,usinipite Nikumbuke,usinipite Uniguze, usinipite Ingawa mi si mkamilifu, usinipite Ah ah, usinipite Natamani nikuone Yesu niguse vazi lako Natamani niwe Batimayo Unifumbue macho Unifundishe maana we mwalimu wa imani Nitapita salama Maana akili zangu zimefika mwisho Tumaini lipo kwako Bwana Na unijaze roho wako mtakatifu Ashike fahamu zangu Nihisi niki kulingana nawe Bwana Maana wajua ninayoyapitia Nahitaji huruma yako Ee Mungu kadiri ya fadhili zako Usinipite Ninaomba Eehh ninaomba neema yako Zaidi nisimame nitangaze Uzuri wako Bwana Yesu unapozuru wengine usinipite Nikumbuke, usinipite Maombi yangu, usinipite Baba uyakumbuke, usinipite Nyakati za majaribu, usinipite Uniguze, usinipite Ingawa mi si mkamilifu, usinipite Ah ah, usinipite Maana hakuna nguvu ipitayo jina lako, usinipite Ni we unaweza, usinipite Navunja maagano yote, usinipite Nikumbuke, usinipite Adui ni mkali, usinipite We Yesu nakuomba, usinipite Ninapokosa tumaini, usinipite Unikumbuke, usinipite Walter
Writer(s): Walter Godfrey Chilambo Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out