Συντελεστές
PERFORMING ARTISTS
Malkia Karen
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Karen Gadner Habbash
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Lizer
Producer
Στίχοι
Ndereno Na Vifijo si Mayowe
Te Amo.. Furaha Yangu Kupendwa Na wewe
Maneno Yasemwayo Nayapuza ujue
Sikurushi roho Nijuache uumie
Na sina sifa ya kuku kila Da ni nipakue mie
Wala Lopo ya Kasuku ya Watu Niyahadithie
Upole wangu Tausi
Vigengeni hunikuti
Na sina Huba la Nuksi
Nakshi zangu Ni Marashi
Sawa Kusemwa Nishazoea
Haya Mwenzako Nishazoea
Sawa kusemwa Nishazoea
Haya Mwenzako nishazoea
Mi sitovaa Vimini vya mpasuo Kwetu Mwiko
Natinga Baibuu Mwilini na Videra Vya Baikoko
Tena Najitia Uturi Viyasmini vya Mtoko
Nikupeleke Nyumbani kisiwa cha Karafuu
Tukale madoriani Shoki shoki za Udambu
Jioni Twende forodhani
Tukale upepo mwanana
Chaza mchukue mwambani
Na iwe zawadi ya mama
Upole wangu Tausi
Vigengeni hunikuti
Na sina Huba la Nuksi
Nakshi zangu Ni Marashi
Sawa Kusemwa Nishazoea (aaah ahhh ah)
Haya Mwenzako Nishazoea (nishazoea mieee)
Sawa kusemwa Nishazoea (oooh ooh oh oh)
Haya Mwenzako nishazoea (nishazoea mieee eeeh )
Written by: Karen Gadner Habbash

