Letras

Hao... hao... Hao... hao... Hao... hao... Hao... Unaona kama kila unachogusa kimeharibika Ujasiri wa kusema tena umetoweka Maana kila unalosema wewe kama unakosea Umechanganyikiwa ni Mungu ajua unayopitia Na ukisema ueleze wengi kwao ni furaha Wewe mwombe Mungu ubaki kimya Na mengi umevumilia, moyo umenyong'onyea Hapo ulipo sasa ng'ang'ania tena Na Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako Imani nusu ongeza utashinda Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako Imani nusu ongeza utashinda. Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yupo nawe Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yupo nawe Moyo wako una majeraha haufaiii Tena unasubiri kauli ya mwisho ya Mungu Wapo wanaojua we huna mtoto Kwa kejeli wanaulizaga ana umri gani Tena wanaojua umefukuzwa kazi Kwa kejeli wanaulizaga bosi wako yupo Ila nakwambia hayatodumu ni nyakati tu Hautobaki hapo hayo ni mapito Jipe moyo tazama juu, mwombe Mungu Ujasiri, Ni mapito tu jipe moyo mkuu Japo huna nguvu yakumwomba mwishie Mungu Ni mapito tu jipe moyo mkuu Mungu hajaruhusu jaribu kuliko uwezo wako, Imani nusu ongeza utashinda Mungu hatoruhusu ufe kabla ya baraka zako, Imani nusu ongeza utashinda Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yupo nawe Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yupo nawe Wewewe Hata wakizusha maneno ya uongo wakakwambia umemwasi Mungu, Ni sawa hawajui unakopita Wakaja na unabii wakasema umefika mwisho wako wee, Ni sawa hawajui unakopita. Ooh wakainuka ndugu wa karibu wakakusema hovyo hovyo hovyo hovyo, Ni sawa hawajui unakopita. Ikawa kila kitu ni kimya marafiki ni kimya Ni sawa hawajui unakopita Kama ndoa ni yako lakini ndani ni uadui Ni sawa hawajui unakopita Ilaaa, Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yuko nawe Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yuko nawe Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yuko nawe Si kwa nyakati za furaha Nawe utacheka tena Usijali Mungu yuko nawe
Writer(s): Goodluck Gozbert Wiki Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out