Créditos
ARTISTAS INTÉRPRETES
Mzee wa Bwax
Intérprete
Shilole
Intérprete
Mohamedi Mwijage
Voz principal
ZUWENA MOHAMEDI
Voz principal
COMPOSICIÓN Y LETRA
ENOCK HAULE
Autoría
Mohamedi Rashidi
Autoría
ZUWENA MOHAMEDI
Autoría
PRODUCCIÓN E INGENIERÍA
MASUDI KANDORO
Producción
Letra
Verse 1
Bwax: Habari yako jirani, vipi umesikia mambo ya mtaa Fulani?
Shishi: Oooh Kwa nini adhalilishwe , kila siku apigike atukanwe na Mumewe?
Bwax: Huo ni Unyanyasaji wa Kijinsia, bila kuchelewa hatua ziweze kuchukuliwa, halafu sio leo tu anampiga na kumnyanyasa, ustawi wa jamii akienda haki atapata.
Shishi: Huku mtaani kuna watu wananyanyasika, huku mtaani kuna watu wanabakwa, huku mtaani kuna watu wana pata shida, ila hawajui wapi wakashtaki wapi.
Bwax: Mbona rahisi wasichokijua kipi, ukinyanyaswa ukipigwa nenda polisi, vituo vya afya ukienda utapokelewa, ustawi wa jamii nako watakusaidia
Chorus:
Unyanyasaji wa Kijinsia, sio ujanja
Unyanyasaji wa Kijinsia, sio ujanja
Kumpiga mtu, kumdhalilisha , sio ujanja
Mtandaoni kuvujisha ngono picha, sio ujanja
Pamoja, tuungane kutokomeza ukatili wa kijinsia
Verse 2:
Shishi: Hebu kwanza nikuulize jirani, kuna aina ngapi za unyanyasaji jamani
Bwax: Zipo nyingi, zote niziweke hadharani, ukatili wa kimwili, ukatili wa kingono, ukatili wa kiuchumi na nyingine ziko kibao. Mimi nakwambia wewe na wewe mwambie yule na yule amwambie yule, na yule awambie wale
Wote: Basi Elimisha, pinga, Tokomeza ukatili wa kijinsia x2
Chorus:
Unyanyasaji wa Kijinsia, sio ujanja
Unyanyasaji wa Kijinsia, sio ujanja
Kumpiga mtu, kumdhalilisha , sio ujanja
Mtandaoni kuvujisha ngono picha, sio ujanja
Pamoja, tuungane kutokomeza ukatili wa kijinsia
Kibwagizo: Jamii isikwepe wala isinyamaze. Toa taarifa kuhusu ukatili wa kijinsia na ukatili wa watoto
Written by: ENOCK HAULE, Mohamedi Rashidi, Zena Yusuf Mohamed

