album cover
Bei
1,075
Afro-Beat
Bei fue lanzado el 13 de mayo de 2026 por Mtafya como parte del álbum Bei - Single
album cover
Más popular
Últimos 7 días
00:40 - 00:45
Bei se descubrió con más frecuencia alrededor de 40 segundos después la canción durante la última semana
00:30
00:40
00:50
02:05
00:00
02:49

Video musical

Video musical

Letra

Vitu vinapanda bei, kila unachokigusa
Bei imekuwa ya moto
Maskini kama mimi ninaejitafuta
Kichwa kinawaka moto
Kila kitu kinapanda bei, usiulize bei
Kinapanda bei, usiulize bei ea
Mfumuko wa bei ya mafuta ni jambo la kidunia
Ila kuna jambo bado nafikilia
Sijui tungepunguza tozo ili tupate ruzuku
Maana mtaani ni mzozo, lipungue hata buku
Maana Zanzibar mafuta elfu tatu lita
Ila Bongo elfu nne mia mbili lita
Sawa kuna vita, ila wapi tunapita?
Serikali ina mkono mrefu ambao sisi hatuwezi kufika
Haya, bidhaa zimepanda, mishahara imeganda
Hatuongei lugha moja, mfano wa Simba na Yanga
Kaka yangu muokota makopo
Analalamika halipandi soko
Mbona sukari ipo juu ya soko
Na mchele upo juu ya soko?
Vitu vinapanda bei, kila unachokigusa
Bei imekuwa ya moto
Maskini kama mimi ninaejitafuta
Kichwa kinawaka moto
Kila kitu kinapanda bei, usiulize bei
Kinapanda bei, usiulize
Kila kitu kinapanda bei, usiulize bei
Kinapanda bei, usiulize bei ea
Wabunge, hivi mnaibana serikali?
Maana huku mtaani ni hatari, hali si shwari
Hospitali mochwari hupewi mwili bila mali
Na wakutusemea ni nyinyi
Wengine wamesoma
Ila mtaani boda boda, na sio boda boda tu
Wanauza hadi mboga mboga
Tumesomeshwa kwa kipato cha elfu moja
Ubishi ndio umetufanya mpaka tumekuwa ma-soja
Kaka yangu muokota makopo
Analalamika halipandi soko
Mbona sukari ipo juu ya soko
Na mchele upo juu ya soko?
Vitu vinapanda bei, kila unachokigusa
Bei imekuwa moto
Maskini kama mimi ninaejitafuta
Kichwa kinawaka moto
Kila kitu kinapanda bei, usiulize bei
Kinapanda bei, usiulize bei
Kila kitu kinapanda bei, usiulize bei
Kinapanda bei, usiulize bei ea
Written by: Mtafya Mwampamba
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...