Paroles

Amen! Amen! (Its new Aloneym pon the track) Mmh nah nah nah, nah nah nah Maisha safari dunia njia tunapita tu Kiachana afadhali ongeza nia utafika tu Walishaniomba lifti kinyonge (Iyee iyee) Nikawapa tafu wasonge (Iyee iyee) Wakaniita kavu mi mnyonge Walonipa ndo wale wale wapora tonge Kodi baba saidia Kwenye miiba palilia Kwenye shimo yafukia Huenda nikapona donda Sina nongwa (Aah), sina choyo Nani mganga aitabiri hii nyota yangu (Aah) Sina meno kibogoyo Mswaki wa nini kinywani mwangu? Wanatamani wanipige hata zongo Kitambi cha masikini kibyongo, wana shombo Maneno neno mengi ya uongo Mpemba nisifike malengo, wanakaba Amen! We omba dua kesho usichoke yatatimia Amen! Weka yako nia Mola wako anakusikia Amen! Fumba macho pia na amini utafanikiwa Amen! Riziki mafungu saba na lako utafikishiwa Walishanitangaza, sambaza Kwa mabaya nikanyimwa mema Wakanipakaza, kujaza Uzuri nimenyimwa sema Pole na unyonge wangu Ngoja binti Juma asante sana mama Salamu ndio natuma nakupenda sana Kwanza moja sio ujinga Ukiamini ipo siku utashinda Japo wapo wanaopinga Pambana, kazana eeh Sina nongwa (Aah), sina choyo Nani mganga aitabiri hii nyota yangu (Aah) Sina meno kibogoyo Mswaki wa nini kinywani mwangu? Wanatamani wanipige hata zongo Kitambi cha masikini kibyongo, wana shombo Maneno neno mengi ya uongo Mpemba nisifike malengo, wanakaba Amen! We omba dua kesho usichoke yatatimia Amen! Weka yako nia Mola wako anakusikia Amen! Fumba macho pia na amini utafanikiwa Amen! Riziki mafungu saba na lako utafikishiwa Amen! Amen! Amen! Amen!
Writer(s): Said Seif Ally Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out