Clip vidéo

Clip vidéo

Crédits

Paroles

Nikifikiria dunia huwaga sipati jibu, nawaza mpaka nadata
Nikikuuliza nini dunia huwezi kunipa jibu, hapo ndo napata utata
Muda mwingine unawezadhani ni utani, mbona vitu vizuri vyote viwe ni vya shetani
Eti mziki shetani, pesa nazo shetani
Mpira na pombe shetani, mademu na mihadarati, shetani
Naamini Mungu yupo najua, ndo ananifanya ninapumua
Akitaka hata sasa atanichukua, ila mi nataka kujua
Ni nini dunia, dunia, dunia,
Hivi ni nini dunia, dunia eeh
Wanaoishi kwa imani, misikitini makanisani
Uwepo wao hauonekani, hali zao zipo taabani
Hivi ulikuaga wapi before, hujaja duniani
Na kwanini kuna kifo, unapokwenda hapajulikani
Sawa safari ni yetu sote, hakuna alokwenda na akarudi
Japo kutusimulia, kama pazuri ama pabaya
Uwe tajiri ama masikini kwa mchanga utarudi
Mi' natoa wosia tusiishi kwa ubaya
Kuna kidude kinaitwa mapenzi, hakijawahi kueleweka
Wakati wewe unalia mwenzako huku anacheka
Hivi ni nini dunia, dunia, dunia
Ni nini dunia, dunia eeh
Tuombeane mwisho mwema (Eeh-eeh yeah)
Tuombeane mwisho mwema (Maana hakuna anaejua kesho)
Tuombeane mwisho mwema (Kama wewe muislamu, omba kwa dini yako)
Tuombeane mwisho mwema (Kama wewe ni mkristo, omba kwa dini yako)
Tuombeane mwisho mwema (Ni siri, ni siri)
Tuombeane mwisho mwema (Ni siri)
Ni nini dunia, dunia, dunia
Hivi ni nini dunia
Written by: Harmonize
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...