गाने

Naitwa Farid Kwa maana mi ni wa pekee na wa aina yake Huu ujasiri na utajiri wa mashairi wa tafsiri zake Jasiri ka usiogope kuumia, ukiwa na noti utumia Kina kinduta, kina pochi wakazia Tajiri wa mashairi mi sio hodari wa kurap tu Mi sio msanii nafanya hii kwa ajili ya watu Nina uso wa mbuzi na ninapewa front page Na daily kwenye news sina skendo yoyote (Wapi, wa.wapi) Wapi niliwakosea? Wapi mie siku-play fair? Sikuzaliwa niwe kamili, nilizaliwa niwe real yeah Na udhaifu hauna dili, kwani strong naji-feel here Nadhifu kiakili, street smart, brush and spear Nipo ili nife maisha sio mchezo wa uoga, mjomba Unataka nshibe hakikisha haukombi mboga, Bomba Nipake tope nijikombe kombe mafuta Uniponde unizonge kutwa Nikonde mnyonge wa kutupwa Kwa mgongo wa chupa nipake nisijepauka Ntaibuka tu kama vumbi dongo likija kukauka Mi nateleza, nakosea Naanguka, napotea Najifunza kuendelea Nainuka natembea Nateleza, nakosea Naanguka, napotea Najifunza kuendelea Nainuka natembea Bendela ya chuma, inapepea Bendela ya chuma Bendela ya chuma, inapepea Bendela ya chuma Nachunga hasira isiniumize ili maumivu yasintishe Hawaishi hila wenye wivu, wanazingira nisipite Dua haziishii angani, ua linazaa bustani Bahati haina ahadi, ikihitaji hutua ndani Sihofii kudondoka sababu mi 'na mabawa Wanaofikiria ntachoka, wanaogopa Ngosha ana Power Cheusi ni mzawa, Cheusi hana dawa ya kutoka Pagawa ukitosa, kosa kunawa kabla haijatosha Kivipi uniache wakati mziki upo na mie? Kwake nina mapenzi ya mswaki Sitaki mwingine achangie Masika bila mbu, sio gharika bila Nuhu Shida nazo kila mtu, chakarika uje unafuu Hekima ni kukosa excuse Kukosa excuse unapo-lose Na pia ukishinda usiji-boost usiji-boo siamini Makuuzi Hekima ni kukosa excuse Kukosa excuse unapo-lose Mi nateleza, nakosea Naanguka, napotea Najifunza kuendelea Nainuka natembea Nateleza, nakosea Naanguka, napotea Najifunza kuendelea Nainuka natembea Bendela ya chuma, inapepea Bendela ya chuma, inapepea Bendela ya chuma, inapepea Bendela ya chuma Nafanya nakaa kama yule MC wa Kenya Ukisikia pah jua haikupangwa ufe mapema Sikuiti shujaa kwa kufanye kile unachofanya Ntakuita mjinga ukiwa ukishindwa wakati Chawezekana Dunia ni kubwa pia ni ndogo ka tukiungana, ki utu Uzima Na mlima haupandwi kwa kuutazama Ningekuwa kisiwa maisha yangekuwa ufukweni Huu upeo nimetunukiwa na Mungu wangu basi Nipokeeni Inatosha? Wanasema hapana, dondosha Na tena wanaochana hawajiiti conscious Ni Ngoshious!
Writer(s): Fareed Kubanda Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out