Lirik

Money makes the world go round Money makes the world go round I say money makes the world go round Money makes the world go round I heard makes the world go round Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes th Ikasikika sauti wananchi tuna msoto na mashaka Pesa imefichwa na kigogo mwenye madaraka Mjira hamna maisha hovyo tumechoka kusafa Na kuanzia sasa tunaingia chocho kwenda kukaba Akapita kibopa mwenye afya Akiwa ana suti kali ni dhahiri ametoka kwenye Hafla Hakusalimia kwakuwa ana kiburi Ila ghafla akajikuta kwenye kona la kibaka Kona la kibaka asiyezubaa hasira imemjaa Amechakaa life imemchapa Kamvaa kibopa kampiga roba matata Pochi ikadondoka muhuni akaokota akachapa raba Masaa kama nane kibaka hajala hata Tumbo linadai na isitoshe jana alilala kapa Akaenda kwa mama Muuza akapiga Nguna Alafu kabla hajasepa akauliza "nikilala huduma nitapata?" Muuza ni dada fulani mwenye bodi tata Kipato hakimtoshi anahitaji kodi ya alipopanga Mwenye nyumba ni mgomvi anahoji anataka mkwanja Anasomesha mtoto Boarding ana boarding wanataka ada Mtoto anayelipiwa ada ye hayuko shule Shule amechoka anatoroka anauza ngada Tatizo lake mzembe alipewa mzigo akaupoteza Na anadaiwa na bosi mtata Sasa ameshahamaki yuko njiapanda Mkono mmoja kwenye kichwa mwingine ameshika ada Anataka kumpa Mtasha anawaza hela haitoshi anaahirisha Anaenda kwa Pusha kuvuta ganja Money makes the world go round Money makes the world go round I say money makes the world go round Money makes the world go round I heard makes the world go round Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes th Anafika kwa Pusha anapewa Kipuli anavuta mastimu anapata Anatoa mpunga ili amlipe pusha Pusha hajainuka mzuka umepanda Pusha kaona Polisi wakuda kama saba Pusha hajaficha Puya anakuta mbwa wametanda Dogo kaangusha mpunga kasepa Pusha kasanda Hawezi furukuta kuruka ukuta kote wamesanda Riziki mafungu saba wanasema Pusha kafunua yote mafungu saba hajapata hata moja Polisi wanaona Pusha hana ujanja Ni aidha waelewane au aende Central akanyee makasha Pusha akaokota mpunga ule mpunga dogo kauacha Akihesabu ni nyingi na bado anatoka kapa Akawaza akimbie labda akaogopa maana Mmoja ameshika Maga kubwa SMG chata Akampa mkuu chake na wale wenzake akawapa Kila mmoja akala zake akaenda zake kudampa Mmoja gambe mwingine anajua kwamba Anahitaji dawa kwa maana mkewe anaugua Kansa Mwingine ni kamali amekubuhu hawezi acha Kufika kwa Sadali kazungukwa na Mashanta Na habari wote tayari wanaijua namba Yaani hata ucheze kwa shari mali hauwezi pata Kila akicheza hola anaokota garasa Akicheki mkwanja unatoka anaanza kuogopa karata Chombo kinaenda mrama, mchuzi umekosa radha Pesa sabuni jamani Polisi akaanza kudata, Coz Money makes the world go round Money makes the world go round I approve that Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes Ikasikika toba tena kwa sauti ya kwanza Wajanja Mkwanja wamekomba na mjinga nauli imekata Maniga wamekomba dola wamezama machaka Na Wasaa wa kugawana chapaa ndio ikawa utata Akasikika dogo " Nawaheshimu sana mabradha " Mnafanya mgao gani ambao siuhafiki hasa Vile mimi ni mdogo mnanifanyia undava Hamuwezi mkagawa kote alafu mimi Mkaniacha Mshata akajibu akasema dogo kausha kwanza Hauwezi ukapaza sauti mahala ambapo hauna chata Hauna ubavu hauna title kauli hauna Kaka Hauna mo Dogo akakunja ndita hasira kushinda Mdada Aliyepima akajikuta na Mimba baada ya kubakwa Gadhabu ya kwanza ishu kuwaza Akakata shauri akachukua kisu akaanza kumfata yule kaka Sauti ya uchungu ikasikika dogo aking'aka Nipeni haki yangu la si hivyo moto utawaka Mkononi zana kali akamfata braza Uku braza anatamba kama ubavu anza kunikata Tumekulea sisi hapa mjini kabla Haujaanza kujua jiji kipindi kaka yako kafa Alileta ujuaji mwingi kama ufanyavyo wewe Tukamchinja mwili Kibiti kichwa Msata Aliishia hapo hakumaliza hata Alichotaka kuongea alitoa macho kama kakabwa Maneno hayatoki tena hali ime-change ghafla Kisu tumboni kauli imekata ndio maana wanasema kuwa Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes the world go round Money makes the world go round So now Money makes the world stops
Writer(s): Edger Vicent Mwaipeta Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out