Lirik

(Wasafi) Sura yake mtaratibu Mwenye macho ya aibu Kumsahau najaribu Ila namkumbuka sana Umbo lake mahbibu Kwenye maradhi alionitibu Siri yangu, ukarimu Bado namkumbuka sana Alionifanya silali (eh) jua kali (eh) Nitafute tukale Lakini hata hakujali, darling Akatekwa na wale Alionifanya silali (eh) jua kali (eh) Nitafute tukale Ila wala hakujali Darling, ah-aah Nitampata wapi, kama yule? Niliompendaga sana Nitampata wapi, kama yule? Nae anipende sana Nitampata wapi, kama yule? Niliompendaga sana Nitampata wapi, kama yule? Nae anipende sana Aii, aii, nyota Nyota ndio tatizo langu Aii, nyota Mpaka nalia pekee yangu Aii, nyota Nyota ndio shida yangu Nyota Wamenizidi wenzangu Alidanganywa na wale (wale) Wenye pesa nyumba ghali (ghali) Mi kapuku hakunijali (jali) Akanimbia, hm Alidanganywa na wale (wale) Wenye pesa nyumba ghali (ghali) Mi mnyonge hakunijali (jali) Akanikimbia Alonifanya silali (eh) jua kali (eh) Nitafute tukale Lakini hata hakujali, darling Akatekwa na wale (halo) Alonifanya silali (eh) jua kali (eh) Nitafute tukale Ila wala hakujali Darling, ah-aah Nitampata wapi? (Oh, wapi?) Kama yule Niliompendaga sana (nampenda sana) Nitampata wapi kama yule (oh, sana) Nae anipende sana Nitampata wapi, kama yule? (Penda sana) Niliompendaga sana (nampenda sana) Nitampata wapi, kama yule? (Oh, sana) Nae anipende sana Bado ananijia ndotoni (bado) Ila nikiamka simwoni (bado) Bado ananijia nikilala (bado) Haki ya Mungu sio masihara Bado ananijia ndotoni (bado) Ila nikiamka simwoni (bado) Bado ananijia nikilala (bado) Haki ya Mungu sio masihara Yo' touch clever (bado) Hii ni sauti ya raisi (bado) Ilomshindaga ibilisi (bado) Kwa mwanadamu sio rahisi, aha Na mwambie (bado) Lazma ujue kutofautisha Kati ya msalaba na jumuilisha Kuna X na kuzidisha Ni cheche (cheche...) Bado ananijia nkilala Haki ya Mungu sio masihara
Writer(s): Naseeb Abdul Juma Issack Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out