Dari

PERFORMING ARTISTS
Zabron Singers
Zabron Singers
Performer
COMPOSITION & LYRICS
JAPHET ZABRON PHILIP
JAPHET ZABRON PHILIP
Songwriter
Emmanuel Zabron Philipo
Emmanuel Zabron Philipo
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Marco Joseph Bukulu
Marco Joseph Bukulu
Producer

Lirik

Ninakumbuka na vazi lake alivovaa wakati akiondoka jana aliniaga akijua atarudi na mpaka sasa hajarudi
Ninakumbuka mipango yake kama rafiki tulisem sema mengi mipango mizuri ya jana na ya kesho yeye
alijua atakuwepo
Ninakumbuka ahadi zake siku ya saba ataanza kuitunza aanze kusali na kimjua Mungu aliamini
atakuwepo
Duniani tunapita tu tusijue kesho itatupa nini hili ni fumbo kaliweka Mungu hivi ni nani ajuae
Bwana ni wewe kutufikisha hapa safari yetu ni wewe(ni wewe Bwana) mtegemewa (hee unatupenda) ni
Maisha yetu ni wewe
Njiani ukasema piteni hapa (wanangu piteni) safari yetu ni wewe (hamtapotea) mtegemewa ni Maisha
yetu ni wewe
Bwana ni wewe umetuleta Baba umetuleta hee umetuleta
Njiani ukasema piteni hapa (wanangu piteni) safari yetu ni wewe (hee nasema piteni) mtegemewa ni
Maisha yetu ni wewe
Maisha ya mwnadamu ni Mungu tu uhakika wa kesho pia ni Mungu maamuzi bado ni Mungu msikilize
Mungu tu
Wataka kuwa sawa anza na Mungu Imani yako wekeza kwa Mungu tu unakesi tubu kwa Mungu badi
fanya ya Mungu tu
NInawakumbuka na wapendwa wetu walio potea na ndoto zao zikazima pia najifunza pekee siwezi bila
wewe Mungu ndo ndoto zangu zitazima.
Duniani tunapita tu tusijue kesho itatupa nini hili ni fumbo kaliweka Mungu hivi ni nani ajuae
Bwana ni wewe kutufikisha hapa safari yetu ni wewe(ni wewe Bwana) mtegemewa (hee unatupenda) ni
Maisha yetu ni wewe
Njiani ukasema piteni hapa (wanangu piteni) safari yetu ni wewe (hamtapotea) mtegemewa ni Maisha
yetu ni wewe
Bwana ni wewe umetuleta Baba umetuleta hee umetuleta
Njiani ukasema piteni hapa (wanangu piteni) safari yetu ni wewe (hee nasema piteni) mtegemewa ni
Maisha yetu ni wewe
Written by: Emmanuel Zabron Philipo, JAPHET ZABRON PHILIP
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...