album cover
Buriani
420
Music
Buriani è stato pubblicato il 23 giugno 2006 da Sony Music Entertainment East Africa come parte dell'album Histori
album cover
AlbumHistori
Data di uscita23 giugno 2006
EtichettaSony Music Entertainment East Africa
Melodicità
Acousticità
Valence
Ballabilità
Energia
BPM78

Video musicale

Video musicale

Crediti

PERFORMING ARTISTS
Juma Nature
Juma Nature
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Paul Peter Matthijsse (P-Funk Majani)
Paul Peter Matthijsse (P-Funk Majani)
Composer
Juma Kassim Ally (Juma Nature)
Juma Kassim Ally (Juma Nature)
Lyrics
PRODUCTION & ENGINEERING
P-Funk Majani
P-Funk Majani
Producer

Testi

Wo wo wo woo
Kifo kifo
Wo wo wowo
Kifo kinatatanisha
Kwanza naanza toa shukurani za rambirambi kwa msiba uliotokea
Hadi baba yetu mkubwa aje kupotea mbele ya macho yetu watoto wake tunalia
Tulikupenda sana upweke umetuachia
Tunaomba japo kidogo sauti kuisikia
Kweli buriani mzee umetangulia ila haya mambo yote mambo ya dunia
Hata Vivi na Complex tulilia
Ndugu majirani nao wanatuhusia
Hapa duniani wote tunapita njia
Huu msiba wako umepunguza nguvu zetu
Kwenye ku fight kazi tunafight peke yetu
Hakuna hata mtu wa kusapoti mambo yetu
Tutaishi kwa amani na upendo baba
Bado tuko pamoja kama watoto na baba
Haitofika siku baba tutakusahau
Ulijitahidi baba kutusomesha
Shule tumefaulu mpaka chuo tumepita
Ndo maana tukifikiri bado tunaona giza
Ila tunajipa moyo kuyakabili maisha
Wo wowo wowo
Kilio
Kifo ndugu yako nani?
Mbona sasa hauonekani?
Kifo ndugu yako nani?
Mbona sasa hauonekani?
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Asanteni kina mama wote mliohuduria kwenye msiba wa baba yetu
Kwa zenu rambirambi na nyimbo za maombolezo
Kutufariji wafiwa kwamba kifo sio kigezo
Tujipe moyo maisha lazima kuwe na mwisho
Yaliyopita si ndwele bora tugange yajayo tu
Mungu akipenda tutaonana tena
Mlaze kwenye kiti baba mahali pema
Ili baraka zake zije kwetu familia
Kila mtu kutaka ufalme wa mbingu kuingia
Mateso ya dunia ye apate kuyajutia
Tizama kila mtu atakuja kwako mola
Bariki mtu wetu mwema mwenye kupenda sala
Alipiga hadithi pindi mi niko chalii
Kukata kata miwa na kugema gema asali
Asubuhi muhogo jioni ugali kisamvu
Maisha tuliyoishi ya shida raha na tabu
Hukutaka kamwe mtoto akakose adabu
Ila hukuwa mwepesi mtotokumpa adhabu
Tulishazoea wajukuu kukuita babu
Sasa watoto wetu wameshamkosa babu
Kilio kilio
Kifo ndugu yako nani?
Mbona sasa hauonekani?
Kifo ndugu yako nani?
Mbona sasa hauonekani?
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Unamchukua kila mmoja kwa style yake
Written by: Eva Butiku, Juma Kassim Ally (Juma Nature), Paul Peter Matthijsse (P-Funk Majani)
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...