album cover
Umaskini
album cover
Umaskini è stato pubblicato il 23 agosto 2026 da Hybrid Music come parte dell'album M.I.L.A.N
23 agosto 2026
EtichettaHybrid Music
LinguaEnglish
BPM77
Melodicità
Acousticità
Valence
Ballabilità
Energia

Testi

hybridbae...
Maisha haya…
Yamechoka mioyo mingi…
Lakini bado tunaamka…
Nimezaliwa kwenye nyumba ya mabati
Mvua ikinyesha maji yana vuja ndani
Mama analia kimya usiku wa manane
Baba amekata tamaa maisha yamembane
Tumekulia kwa njaa hadi tumeyazoea
Chakula ni bahati siku nyingine patupu juu ya meza
Viatu vya shule vilipasuka zamani
Lakini bado nilitembea kilomita nyingi
Watu wanatudharau kwa nguo tulizovaa
Mikono mifukoni hakuna hata mia
Tulibeg barabarani ili tupate chai
Lakini wengine walituona kama hatufai
Umaskini ehhh… unauma moyoni
Kila siku ni kilio ndani ya roho zetu
Umaskini ehhh… unaua taratibu
Ndoto zinafifia gizani kimya kimya
Tulikesha na njaa
Tukaomba msaada
Lakini dunia ikatupita tu…
Kuna siku tulilala bila hata maji
Tumbo linauma lakini hakuna chochote ndani
Mama akauza nguo ili tupate unga
Kesho yake tena tukarudi kuomba
Marafiki walitukimbia polepole
Walipoona maisha yetu hayana mbele
Mapenzi nayo yakawa ni mateso
Maskini ukipenda unaonekana mchezo
Tulitamani maisha ya kawaida
Kuvaa vizuri na kuishi bila shida
Lakini pesa ikawa kama ndoto mbali
Kila tukijaribu maisha yanatuangusha chini
Lakini maskini pia ana moyo…
Anaumia…
Anaota…
Anaomba siku moja abadilishe maisha…
Usimdharau maskini…
Huenda kesho akawa juu kuliko wewe…
Umaskini ehhh… umetufundisha mengi
Kuvumilia maumivu ya dunia hii
Umaskini ehhh… machozi yasiyoisha
Lakini bado tunaishi kwa matumaini
Bado tunaamka…
Bado tunaomba…
Bado tunaamini…
Siku moja… maisha yatabadilika…
Written by: Milan Aboud Aboud
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...