歌詞

Sasa unanuna nini? Au unadhani hata mimi napenda Nishazichoka na mimi Mboga za majani kila siku mlenda Siko juu siko chini Niko nusu sadoo Sio wa kumi si sabini Ngoma ngumu bado Kama ibada naswali sana Usiku wa manane Tena nafunga na Suna Mambo bado bado mwana wane Naona yanazidi kuguma Nikirudi na hasira hasira (nizoee) Mambo magumu bado bila bila (niombee) Nikirudi na hasira hasira (nizoee) Mambo magumu bado bila bila (niombee) Halijakaa sawa Nivumilie ipo siku tutapata Halijakaa sawa Shida na dhiki zitakwisha baby Halijakaa sawa Kuchana kope make up utapaka Halijakaa sawa Tutabadili mboga kuku kwa manyama Chochea kuni kipenzi changu Asubuhi tumbo likikuming'inya Pokea kidogo changu Tunywe chai na mkate wa kumimina Akili ikichoka riziki nikikosa Najua kwako nitajiliwaza Kama makosa nivute chumbani Kununa nuna unajilemaza Ustahimilivu mnao wachache mno Jua shida rafiki wa mbivu Baada ya dhiki mavuno Kila jema lina maumivu Na kwenye waliopo tumo Yarabi salama tupe tulivu Penzi lisifike kikomo Iyee eeh eeh Nikirudi na hasira hasira (nizoee) Mambo magumu bado bila bila (niombee) Nikirudi na hasira hasira (nizoee) Mambo magumu bado bila bila (niombee) Halijakaa sawa Nivumilie ipo siku tutapata Halijakaa sawa Shida na dhiki zitakwisha baby Halijakaa sawa Kuchana kope make up utapaka Halijakaa sawa Tutabadili mboga kuku kwa manyama
Writer(s): Sheila Shorongo Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out