ミュージックビデオ
ミュージックビデオ
クレジット
PERFORMING ARTISTS
Young Lunya
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Rashid Shabani
Composer
PRODUCTION & ENGINEERING
Daudi Bakari Myoya
Producer
歌詞
[Intro]
Kichwa kina vitu vingi ila haimaanishi sikupendi
Ni vitu vingi tu, ila haimaanishi sikupendi
[Chorus]
Kichwa kina vitu vingi ila haimaanishi sikupendi
Sitabiliki siambiliki ila haimaanishi sikupendi eh
Shoga zako, wana tabia za kishenzi
Wananipakazia maushenzi ila haimaanishi sikupendi uh
Kichwa kina vitu vingi eeh
Ila haimaanishi sikupendi baaw
Sitabiliki siambiliki ila haimaanishi sikupendi uuh
Shoga aah, zako eeh wana tabia za kishenzi hee!
Wananipakazia maushenzi baaw
Ila haimaanishi sikupendi skkkkrrrr
[Verse 1]
Natoka nyumbani kwenda kutafuta ili nyumbani tusile dagaa
Muda ni mchache mambo ni mengi staki mtoto ulale na njaa
Pilka pilka tunapigika na sio kitoto balaa balaa
Na sie wengine sio wakishua vyema kwenda kupigana na mtaa
So penya penya ka pikipiki
Leta Burger na vichips chips
Na tukuku kuku koni pipipipi
Na matunda tunda ndizi matikiti
Na vijiti vipi?
Kila ninachofanya unakijua ntakucheati vipi
Shoga zako wanaojifanya hawanipendi
Hao ndo ambao wanauzimia mziki
Na siwapi nafasi, nawalia bati
Mademu wengine wa nini kujifanya mswati
Ndo maana sa ingine natoka nyumbani
Nasahau hata kupiga mswaki
Na muda mwengine sitoi hata kodi ya meza
Natoka kibati
Hapo utashindia mandazi
Ila nikirudi ni party
[Bridge]
Wengine wanasema nawataka
Ila wao ndo wamejaa kwenye DM
Na wala hawachezei block
Ila najifanya I don't see em
Wajuze ya kwamba siwezi kujigawa
Moyo wangu upo kwako waambie
Mimi ni wa kwako waambie
Wewe ni wa kwangu ndo kiboko ya mie
[Chorus]
Kichwa kina vitu vingi ila haimaanishi sikupendi
Sitabiliki siambiliki ila haimaanishi sikupendi eh
Shoga zako, wana tabia za kishenzi
Wananipakazia maushenzi ila haimaanishi sikupendi uh
Kichwa kina vitu vingi eeh
Ila haimaanishi sikupendi baaw
Sitabiliki siambiliki ila haimaanishi sikupendi uuh
Shoga aah, zako eeh wana tabia za kishenzi hee!
Wananipakazia maushenzi baaw
Ila aimaanishi sikupendi skkkkrrrr
[Verse 2]
Kukupoteza wewe, siwezi kubali
Kitu kingine nnachokipenda unanikubali
Alafu mwenyewe unajikubali
Sie tuna kitu tutafika mbali
Nitakupeleka kwa mama akakuone nimepata mwali
Sasa muda mwengine kichwa
Kinapata moto maana
Hata ukitazama simu haziiti
So inanibidi nipanguse chanda
Pesa kwenda kuzitafta kibishi
Nitajua mbivu nitajua mbichi
Nawe nakujua unavyopenda maupishi
Nywele pochi out kila week
Sasa, kwa kipato gani cha mziki!?
Maneno hayakosi yapuuze mpaka wakuone una nyodo
Nami sikuachi chini ya mpera nimeokota dodo
Action nyingi maneno kidogo
Maskio hayataki tena kuskiza zogo
Bize kama tunakata gogo
Ndoto haziwezi kutimia kama mwendo ni mdogo
Walikuja wenye magari na nyumba na hawakukupata
Sasa inabidi nipambane kukupa chochote utakachokitaka
Iphone sijui nini vitakaataka
Nilete chochote utakachotaka
Ndo maana nakwenda mchaka, ili baby akiitaka, baby anaipata
[Bridge]
Wengine wanasema nawataka
Ila wao ndo wamejaa kwenye DM
Na wala hawachezei block
Ila najifanya I don't see em
Wajuze ya kwamba siwezi kujigawa
Moyo wangu upo kwako waambie
Mimi ni wa kwako waambie
Wewe ni wa kwangu ndo kiboko ya mie
[Chorus]
Kichwa kina vitu vingi ila haimaanishi sikupendi
Sitabiliki siambiliki ila haimaanishi sikupendi eh
Shoga zako, wana tabia za kishenzi
Wananipakazia maushenzi ila haimaanishi sikupendi uh
Kichwa kina vitu vingi eeh
Ila haimaanishi sikupendi baaw
Sitabiliki siambiliki ila haimaanishi sikupendi uuh
Shoga aah, zako eeh wana tabia za kishenzi hee!
Wananipakazia maushenzi baaw
Ila aimaanishi sikupendi skkkkrrrr
Written by: Rashid Shabani