ミュージックビデオ

ミュージックビデオ

クレジット

PERFORMING ARTISTS
Dizasta Vina
Dizasta Vina
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Edger Vicent mwaipeta
Edger Vicent mwaipeta
Songwriter

歌詞

VERSE I
Sitauona uzuri wa mataa
Maua na uturi au usafi wa suti nitayoivaa
Mtajadili kama nilifunzwa chuki na hii njaa
Au msamaha niliomba baada ya kuivunja mioyo kadhaa
Mikono yangu haitaishika sayari
Historia nitakuwa nimeimaliza tayari
Naenda upande wa pili, asili itanipiga kabali
Nitakuwa nimeimaliza safari
Maombi hayatakidhi nisimame soja
Nanyi mtaijua hadithi hii ya upande mmoja
Pesa na ustaa hautanibeba
Itaandikwa "mwisho wa kila shujaa ni jeneza"
Siwezi kimbia udhuru hata nikibadili njia
Nakuwa huru dhidi ya kufuru za hii dunia
Mwangaza hautafika himaya yangu
Je mtafurahi nikifa ama mtaliimba jina langu?
Siku hii iwakumbushe kuwa kesho mbali
Iwakumbushe havina maana pesa mjengo mkali
Vyeo urembo na pesa nyingi
Ni kiburi cha hii pumzi, pumzi ambayo ni temporary
Sijui Nitamwachia nani mama yangu
Ikiwa, nitaacha dini, itikadi ya chama changu
Cheo changu hakitakuwa na maana tena
Nitalala gizani japo mtajua nimelala pema
CHORUS
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia...
VERSE II
Nitalala sitahisia karaha zako
Sitasikia matusi sitasikia msamaha wako
Sitasikia kicheko au kilio cha unafiki
Ubongo hautatafsiri mawimbi ya sauti yako
Nini maana ya chuki yako kwangu ikiwa
Siwezi amka hayafungukia macho yangu
Nitakuwa mbali peke yangu futi sita
Hata kivuli hakiwezi kuwepo kando yangu
Ufedhuli ni kibari cha hii nguvu
Ya nyama na mifupa ambayo ni mali ya wadudu
Ipo siku utaimbiwa pambio na wadau
Kisha Ndugu watagawana salio na kusahau
So, nataka nikifa msinidai
Msilie msherehekee niliyoyafanya nikiwa hai
I wonder kama mwangaza usipotimba himaya yangu
Je utafurahi nikifa ama utaliimba jina langu?
Minara yangu imara itadondoka nayo
Sauti yangu ya gharama nitaondoka nayo
Masikini roho yangu mimi
Itaenda wapi pindi mwili utakapogusa
Udongo mkavu chini
Mwangaza hautafika himaya yangu
Je mtafurahi nikifa, ama mtaliimba jina langu?
BRIDGE
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi...
CHORUS
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia...
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi
(Dunia inashindwa kunilinda)
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi
(ni dhaifu na kweli)
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia...
Written by: Edger Vicent mwaipeta
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...