album cover
Aah Wapi
1,811
Music
Aah Wapi은(는) 앨범에 수록된 곡으로 2003년 12월 12일일에 Sony Music Entertainment East Africa에서 발매되었습니다.Ugali
album cover
앨범Ugali
발매일2003년 12월 12일
라벨Sony Music Entertainment East Africa
멜로디에 강한 음악
어쿠스틱 악기 중심
발랑스
춤추기 좋은 음악
에너지
BPM92

크레딧

실연 아티스트
Juma Nature
Juma Nature
실연자
작곡 및 작사
Paul Peter Matthijsse (P-Funk Majani)
Paul Peter Matthijsse (P-Funk Majani)
작곡가
Juma Kassim Ally (Juma Nature)
Juma Kassim Ally (Juma Nature)
가사
프로덕션 및 엔지니어링
P-Funk Majani
P-Funk Majani
프로듀서

가사

Sijui kama itawezekana (aah wapi)
Mtu niliyempenda sana (aah wapi)
Tukaja tukafarakana (aah wapi)
Sababu wanachonga sana (aah wapi)
Sijui kama itawezekana (aah wapi)
Mtu niliyempenda sana (aah wapi)
Tukaja tukafarakana (aah wapi)
Sababu wanachongasana (aah wapi)
Kuna mambo mwera huwa siyahusudu
Ni sawasawa na yale ambayo huwa wanafanya wadudu
Wadudu walio wengi na hasa wale waharibufu
Washazoea umbea fitna na kujenga bifu
Wanafanya uchunguzi kutoa wanaogopa tifu
Si migazeti mingine inalaani kuwa mtulivu
Nilichogundua mimi kumbe inataka iuze
Hii naitoa live na nataka mjifunze
Sasa hivi tutakatana mapanga siku ambayo nitachoka
Mbona nyinyi hamjiandiki kuwa mnabaka dada zetu?
Kila siku niache demu alienipenda niliempenda
Nikijiskia uchovu tu ananipa denda
Ananipa ushauri vipi biashara inakwenda
Hata mnichome moto kwanza kuniua ni kama ndoto
Mtakufa na viburi vyenu vya roho mlionavyo hivyo
Wengine ni mijamaa ambayo kila siku ina wivu
Wanataka wanipotoshe niwafate wengine niwe jivu
Nimewashtukia hamnipati ng’o
Tabia hazilingani mbinguni moto wa kijani
Mtawezaje kutuzuia jama kwani kitu gani?
Wako kama wangu kwanini ummezee mate?
Halafu nikipita mimi kwanini unatema mate?
Mwingine anakukuta upo kwenye mood nyingine
Halafu yeyeanakupa story nyingine
Wengine wananong’onezana mimate wanatemeana
Sijui kwanini wengine wanakuaga ni wambea
Mtavalishwa kanga shauri yenu
Halafu muanze kupita njiani halo halo
Mwanamke kuupara babu wee
Niachie mimi msela mgumu mwenye kuukaanga mbuyu
Mi ndo nshashinda niacheni mwenye meno nitafune
Vigenge havisaidii maneno muongeze bidii
Mnaweza mkajitahidi hebu ongezeni ongezeni bidii
Hata mjaze gunia la maneno siwasikilizi ng’o
Sijui kama itawezekana (aah wapi)
Mtu niliyempenda sana (aah wapi)
Tukaja tukafarakana (aah wapi)
Sababu wanachonga sana (aah wapi)
Sijui kama itawezekana (aah wapi)
Mtu niliyempenda sana (aah wapi)
Tukaja tukafarakana (aah wapi)
Sababu wanachonga sana (aah wapi)
Mwanamke wa bongo sharti umgharamie
Usipomgharamia wenye vitambi watakuchukulia
We unafikiri mwanamke wako atavumilia
Kuwaona mashoga zake mtaani wakimtanulia
Mwenzie *** kanunuliwa cheni ya dhahabu
Halafu kila jumapili tunaenda kumcheki muumini
Habari ndio hiyo washkaji hata mkinuna
Ni ngumu kuliacha baga wakati njaa inakubamiza
Unajaa uko ndefu kuanzia asubuhi hujaingiza
Na baga haina uchu kama utamu wa sambusa
Nimuache demu wako eti kisa kasema musa?
Musa si kama paka kila kitu ananusa
Yameshamshinda yake sasa anafata ya wenzake
Midemu iko mingi kama bilioni ishirini na tisa
Lakini nikitaka kuwafata tu roho yangu inasita
Yote ni shauri ya upendo wa kweli mkimind mtakufa
Wabongo sjui vipi hatuskii kivipi vipi
Jana kulikua na mtu amekufa kwasababu ya ngoma
Nikajivuta ili na mi niweze kuona
Ana ngoma ana ngoma wallahi hatopona
Alikufa na vikunyanzi utadhani mwili ameshona
Sasa faida iko wapi mbona mnanifata fata jama?
Niacheni na huyu ambae mnaniona kuwa chizi
Siwezi kumuacha kamwe nimfate nyambizi
Eti demu wako hafai hafaihafai
Na tena haongei hayo akiwa amekunywa pombe
Mtu mzima ana ndevu za osama lakini aibu hana
Si useme tu unatafuta njia tuachane
Ili umchukue mkale ndege mjichane
Acheni wivu wa sifa demu hataki *** kushika
Wengine mnazoza eti demu ana mimba
Ulimpa wewe??
Wengine wanasema hanipendi anataka mavumba
Wakati wako haujafika ukifika ntakutaarifu mdanganyifu mkubwa we
Tena hufai
Sijui kama itawezekana (aah wapi)
Mtu niliyempenda sana (aah wapi)
Tukaja tukafarakana (aah wapi)
Sababu wanachonga sana (aah wapi)
Sijui kama itawezekana (aah wapi)
Mtu niliyempenda sana (aah wapi)
Tukaja tukafarakana (aah wapi)
Sababu wanachonga sana (aah wapi)
Written by: Juma Kassim Ally (Juma Nature), Paul Peter Matthijsse (P-Funk Majani)
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...