Songteksten

Oh oh oh...! Salome juu ya kaburi lako nalia aaa! Kilio nakisikia, dakika za mwisho Mpenzi wangu najutiaa kosa nilokufanyiaa Siku ya kwanza nilikutana na wewe Akili iliruka na kupata kiwewe Sikuamini kama ningekutana na wewe Hilo la kwanza naomba unielewe Nikakutongoza ukanikubalia Ulijipa moyo tena mia kwa mia Umekwishapata bwana atakayekuoa Kumbe nilikuona kama demu wa kuzugiaa Miezi saba mbele iliendelea Na mapenzi kwako wee yakapungua Kumbe ulikuwa na mimba ya kujifungua Miezi yote hiyo wala hukuniambia Ulijua lazima nitaisaigia Na ndio ndoto yangu hiyo ilikuwa Na ulipojaribu mimi kuniambia Katukatu nami nikakutalia Salome mpenzi wangu ukaanza kulia Kwa uoga wangu mimi nikakuambia Tuonane siku inayofuatia Kwa unyonge Salome ukaitikia Salome juu ya kaburi lako nalia aaa! Kilio nakisikia, dakika za mwisho Mpenzi wangu najutiaa kosa nilokufanyiaa Siku ya pili tena ilipofikia Asubuhi mapema ni-nikakimbia Nikakimbia kuelekea Mbeya Huku nyuma Salome uliningojea Saa dakika, sekunde zilipotokea Ulichoka mpenzi kwa kuningojea Ikabidi uje kuniulizia Nyumbani wakesema Dully ameshakimbia Salome mpenzi wangu ulinyong'onyea Hazikupita dakikaa ukazimia Ndoo za maji tatu wakakumwagia Ndipo hapo fahamu zikakurudia Ulilia mwishowe mpaka kujutia Ulijuta kwa nini ulikunikubalia Ulirudi nyumbani kwenu unalia Hadi chumbani kwako ukajifungia Salome mpenzi wangu ukaandika barua "Msifunge Dully mimi najiua" Dakika tano mbele zilipowadia Polepole kitanzi ukajifungia Ukajinyonga na kuiaga dunia Nisamehe Salome leo najutia Ukajinyonga na kuiaga dunia Nisameheee Salome leo najutia Salome juu ya kaburi lako nalia aaa! Kilio nakisikia, dakika za mwisho Mpenzi wangu najutiaa kosa nilokufanyiaa
Writer(s): Trabye Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out