Tekst Utworu

Eeeh eeh Roho yangu kama itakusaidia (ndugu yangu) kama itakupa ushindi Moyo wako najua Kama itakusaidia kama itakupa ushindi moyo wako najua Usiku rafikibwa giza Basi njoo uichukue×3 Uichukue Basi njoo uichukue×3 Ama kweli kama hujui unapo kwenda huwez kupotea na watu kukimbia wanakozika hudondokea kwenye mait nyama. Siku zote naamin mtu huwez kulala kwenye mto hata kama umekauka Na ukitaka kujua mwendo wa mjinga mpe kilemba uone Hili niombi langu toka kwangu kuja kwako Kama ya kwangu itakusaidia chochote kwenye ushindi wako niko tayari kukupa ila uifuate nyumban wala sio mbali! Nakukumbusha ukitaka n'zi wasikufuate achakula vilivyooza chuki humchoma aliyeihifadhi kwenye moyo tu siku zote Nakuuliza unatak kuja mchana ama jioni maana kila njia na muda wake najua mara nyingi ungependa kuja mchana ili uenekane Naomba nikuelekeze hivi pita uwanja wa taka hadi mfereji mchafu Kisha kibanda cha mbavu za mbwa katiza usisikie na mtu njiani endelea kuja Ni kioo tu pekee yake ndo huonyesha doa la kwel kwenye paji la uso Katiza choo cha gunia pembeni maskani camp Taliban camp Ukisikia harufu kali bana pua haraka hapo choo kinapakuliwa na kutia moyo tu njoo karibia unakaribia kufika Kama itakusaidia (itakusaidia) kama itakupa ushindi(moyo wako najua)×2 Usiku rafiki wa giza Uliza baba ubaya aliyetoroka jela au mama Mwantum anayesutwa kila kukicha Ukiogopa kupotea uliza babu Nshuba kikongwe muuza bangi atakupa uchochoro utapita ubavu ubavu Kila hatua utakayopiga kumbuka maji ya dafu hayanywei kwenye glass na siku hizi kinachopandwa kwenye changarawe kinakua haraka kuliko kwenye udongo Nakuomba ukisikia kuntumtututu ujue kuna mtu anachezwa endelea kuja na ukisikia cherekooo watu wanasasambua endelea unakaribia Alama kubwa utakazokutana nazo ni visheti na chips dume, kashata na maandazi, chapati na uroge wa ubuyu, pweza na vijit vyake Ukiona sufuria la supu unakaribia maana nchi yenu nchi yetu pia hapa watu pale kinyesi na kondom ndo kwetu dampo dogo pale pembeni maji ya mtungi nyumbani huko Chumba cha baba hapa choo cha pipa pembeni Unakaribia Usiponikuta jua ya kwamba nipo ferry kuungaunga mwana kwenye samaki anayechafua anasafisha kwa kutupa hana hapo sasa umefika Vipi bado unaitaka na ya kwangu ikuongezee ushindi kama ndio kuna masharti mawili tu Pitia kwa yule mama kamuombe samahani na uumpe pole kwasababu kwa kauli zako alipoteza kitanda chake Na kwenye hela mkiweka picha zenu wekeni na za kwetu wakati mnatumia mtutumia na sisi Mwisho lakini sio kwa umuhimu kwenye kiapo chako cha kweli ongeza na majina yetu Basi njoo uichukue Basi njoo uichukue Basi njoo uichukue(roho yangu)uichukue Basi njoo uichukue Basi njoo uichukue Basi njoooo uichukue(Roho yangu) Basi njoo uichukue uichukue Basi njoooooooooooooooo
Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out