Letra

Naogopa nikiwaambia watu sijui wataniona vipi Naogopa kuyasema yote acha tu ninyamaze kimya Naogopa kuwaambia watu wanaanza kunisengenya Nina maswali mengi, miguuni Pako Kwa nini Mungu, umekuwa kama vile huoni? Pesa sina, lakini umeacha niugue Namtegemea lakini umemwacha aondoke Kwa nini Mungu umenyamaza? Mawimbi ni makali, upepo ni mkali na mlima ni mkali Umenyamaza Maumivu ni makali na vita ni vikali Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu Mawimbi ni makali, upepo ni mkali na mlima ni mkali Umenyamaza Maumivu ni makali na vita ni vikali Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu Mbona kwa yule Ulitenda juzi, na leo tena Una ugumu gani kwangu Baba, sema basi Mimi binadamu nakosa majibu, sema Baba Nakuamini sana Baba yangu, Usiniache Kuna shida gani, imekuwaje? Hata Usiseme Kama ni kosa naomba Unisamehe Urekebishe naomba Unisamehe Nateta Nawe sitokata tamaa Wa kuamua yangu bado ni We Nakuamini Mungu bado ni We Naogopa uko kimya kuna nini Mungu? Sema neno Usikae kimya Mi'sijakufuru Mungu Kama siku zangu za kuishi duniani bado zipo Naomba sasa Baba Umalize, Umalizane na shida zangu Mambo mengi nimeomba Kwako Umejibu, hili hujajibu Mungu wangu, bado nasubiri Kwako Jibu basi, watu wakuone Wewe Watu wakuone Baba Bado nasubiri Kwako Mawimbi ni makali, upepo ni mkali na mlima ni mkali Umenyamaza Maumivu ni makali na vita ni vikali Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu Maumivu ni makali na vita ni vikali Nimevumilia nimeshindwa, sema kitu
Writer(s): Maureen Nkirote Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out