Letra

It's Bob Manecky Iyee, iyee iye eh Iwe kibatari, ama mwanga wa mshumaa Kwenye kigiza cha jioni Pika dona ngangari, tulishushie na dagaa Ukishatoka sokoni Kisha tufunge safari, itayochukua masaa Utokwe jasho mgongoni Na vile 'na machachari Nikikushika Kibaha, utamu hadi Kinondoni Kuna muda nawaza, hivi nitakupa nini? Sina mbele sina nyuma masikini Chakula shida na tunalala chini, nambie Wenye mapesa, Vogue na ma-Lamborghini Wasijefanya ukanipiga chini Bado nawaza, hivi nitakupa nini utulie? Sambusa, kachori, bamia (aah) Tukipata pesa ni sangara Mchicha, mtori, bamia (aah) Kama tukikosa tunalala Kwa hiyo mama usijali, vumilia (iye eh) Vumilia (iyee ye) Vumilia, kesho tutapata mpenzi Vumilia (vumilia) Vumilia (vumilia) Vumilia, kesho tutapata mpenzi Najua unatamani high waist, make up Weaving za Dubai na China Ule pamba nyepesi, setup Cheni ya dhahabu yenye jina Basi mama vumilia, nakupigania, mpenzi subiria Acha kujiinamia, punguza kulia, atatusaidia Eti mapenzi si moyo, mapenzi ni pesa Ama kweli masikini yatatutesa Uchoyo, usinipe presha Naomba unipende Kuna muda nawaza, hivi nitakupa nini? Sina mbele sina nyuma masikini Chakula shida na tunalala chini, nambie Wenye mapesa, Vogue na ma-Lamborghini Wasije fanya ukanipiga chini Bado nawaza, hivi nitakupa nini utulie? Sambusa, kachori, bamia Tukipata pesa ni sangara Mchicha, mtori, bamia Kama tukikosa tunalala Kwa hiyo mama usijali, vumilia (iye eh) Vumilia (iyee ye) Vumilia, kesho tutapata mpenzi Vumilia (vumilia) Vumilia (vumilia) Vumilia, kesho tutapata mpenzi
Writer(s): Raymond Mwakyusa, Rayvanny Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out