Letra

Haliya kuwa nimebaki mwenyewe Sina hili wala lile Nimekuwa kama zoba nimezubaa Kama ni kuku kifaranga kwa mwewe Ataenda huku ataenda kule Atapigwa roba atasombwa Nimemuachia ushindi Japo mi ndo nimeshinda Nimenawa basi Nenda mama nenda Mtu umekaa huna amani Hakuba mapenzi atakupa nani Sahani yake ipo sokoni Yanunuliwa kama nyama buchani Nimemuachia ushindi Japo mi ndo nimeshinda Nimenawa basi Nenda mama nenda Nitamsemea wapi Hata ndugu yake mmoja sikumjua Nitamsemea wapi Ohhh ohh oh Nitamsemea wapi Naona joto naona baridi Nitamsemea wapi Leo nafungua koo Nishaumia sana roho Yanini nikae nayo Na yananitesa Ogopa chozi linalotoka Likimtaka Mungu aje asaidie Binadamu akishindwa Kibao kimegeukia kusini Maneno juu chini hayasomeki Upepo mkali ila bendera haipepei Mapenzi yana nguvu ya ziada Nimemuachia ushindi Japo mi ndo nimeshinda Nimenawa basi Nenda mama nenda Nitamsemea wapi Hata ndugu yake mmoja sikumjua Nitamsemea wapi Ohhh ohh oh Nitamsemea wapi Naona joto naona baridi Nitamsemea wapi
Writer(s): Frank Ngumbuchi Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out