Letra

Umepika chakula huli, huoni chapoa? Umpweke, mwenye moyo wa duni, twakuita soledad Kula dada kwani huyo haji, eti yuko na washikaji Na akirudi matokeo yake ugomvi hauishi Uko alipo mbali na upeo wa macho yako Atafanya baya atakalo bila idhini yako Unangoja na kusubiri, utasubiri sana Hatokeo kwako machoni hutomuona mwenzio Uko na rafiki zako, kwako nyumbani kitako Mkipeana michapo, huku mkicheka na vicheko oh Wawapa habari zako, jinsi bwana anavyokutenda Hutojua moyo wake, kwani ni vigumu kufungua moyo Usijigambe ye akupenda Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako We wampenda Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woo Mmelala ni usiku sana, usiku wa manane Akili yake kumbe yamuwaza akiwa na mwingine Milio ya simu na ujumbe mfupi vinazidi kwa sana Ukimuuliza bwana kulikoni utaambiwa ni story Nao moyo wako punde, unaanza kwenda mbio Mara usiku akuage kuwa anakwenda kutukio Muulize ni wapi pande, hatokujibu mwenzio Mara na siku zingine simu yake iko bize nusu saa Usijigambe ye akupenda Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako We wampenda Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woo Angeujali moyo wako, asingekuumiza huyo Angeacha atendayo ili wewe upate faraja ah Lakini umuulizapo, juu yeye hukujia Hathamini chozi lako, na wala halijali hilo lako pendo Usijigambe ye akupenda Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako We wampenda Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woo Usijigambe ye akupenda Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako We wampenda Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woo
Writer(s): Lady Jay Dee Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out