Lyrics

Ah! Nilipaa sasa natua Kwenye, kwenye Siri ya moyo Na siri ya moyo Anayeijua mwenye Mwenye ujasiri wa Kutunza nafanya Ninachodhani ni Sahihi kitachotokea Nitajua mbele Wanasema mwanaharamu Haijui laana, kashalaanika Nasikitika kuwa haujui Kama naonekana ka' Kondoo kwa mchungaji Lakini... lakini kwa ndani Mi' ni chui mama Kwa mfano nakuita mpenzi Na tabasamu zuri wakati Najua kuwa sikupendi Kuitoa hii siri ndo' siwezi Kwahiyo nitakudanganya Mpaka ifike siku niutimize Ushenzi Huwa nawaza nikuweke Ufahamu,mtambue Kuwa mpo wengi Na lengo niwateke Ili mpeleke salamu Masikini mrembo Nashangaa jinsi unavo'ngoja Pete kwa hamu Vile hunioni kwenye Makundi ya baa Na bahati nzuri haujawahi Kusikia nikizushiwa uzushi Kumbe unampigia mbuzi gitaa Sometimes unanisongea nguna Au wali ukidhani mi' najali ilihali Sina habari, sina hisia siwazi Hata kukuonea huruma Na sibadili dhambi hata Mbingu ikisogea nyuma Ah! Nashiriki nawe nyakati Twitter mpaka instagram Picha unani-hashtag drunk in love Nanunua brand za gharama za Simu ya ghali breakfast Zanzibar Haimaanishi kuwa Tunaianza safari Nataka nikuandalie maumivu Ili kila unachokiona Kiwe kinafanya unikumbuke Ni hatari Inaitwa zuia nanga kabla Bado haijang'oa Maana haujaheshimu Mvua kama bado hujaloa Kwa huu mchango ninaotoa Ndo' unafanya unazama Zaidi kiasi unaiwaza mipango Ya ndoa Jicho la tatu hauna Fungua jicho lako la pili Utagundua kila ninachofanya Ndo' maana haujaona bado Wala haupo kwenye Mpango wa pili Ah!! Unaniletea zawadi toka Nilishawaacha Na walinichora tattoo Mi sio tunda mama Mama mi' kidonda Utachelewa kusonga Ka' bado unaingoja nafuu Sherehe ya birthday yako Kwenye 'temple' ya anasa Umekuwa 'mental' kwa Huu mwendo ndo' Umenasa Kiasi unahisi huu ni upendo Tukishiriki tendo tu nakuacha Kichwa changu hichi, kichwa Nitalala na wewe na Wewe na haifiki jumapili Nitakuwa nimeshakuacha Ah! utanitafuta Kwenye simu ambayo Namba nitakuwa nishaibadili Utanitafuta mara mbili Mara tatu kisha nne Utagundua kurudi Itang'ata moyo wako Watu maumivu Hukujiandaa kuyakabili Utanipamba majina ya Nitakuwa mbali nishasafiri Nishasahau utatunga nahau Wakati haukuwahi kuutabiri Ila upo Utaumia utashindwa kusimulia Utaniulizia kwa wanaonijua Hauna tena chako Okota vipande vya moyo wako Nenda zako kaandike Tanzia Kisha watajua wenzio Wanafiki watacheka Wanaokujali wataangua kilio Watakusindikiza kulia Watakupa pole wengine watasema Wanaume wote mbwa Taswira itazongwa Na wingu Picha utazichoma Kwa kisu Utanitukana mara mwana Haramu mara malaya Rafiki zako wakuu watakuwa Filamu na riwaya Wimbo niliokuimbia Kamwe hautokukonga Utachoma mkuki moyoni Kisha kunyonga Utaendelea kungoja Utagundua mvumilivu Hali mbivu hiyo Methali iliongopa Utagundua ilikuwa Ni soga Hii itafanya ukonde Na kuanza Kutumia pombe na ganja Nayajua haya yote Kwa maana ndo nilikotoka Utasimama kijasiri Na mwisho utadondoka 'Sikiliza' Wataleta daktari Akuulize nini shida Hawatapata Jawabu kabisa Wataleta sheikh Wataleta mchungaji Wa kanisa Watasahau kwamba Moyo uliovunjika Hauna tiba Natamani nikuambie kuwa nimekuteka makusudi Maana unasikia na hujifunzi Nikuumize kama mke wangu mpuuzi Aliyekimbia na rafiki yangu siku moja baada ya harusi Nilishaambiwa na Mama nikapuuzia Kuwa haujawahi Kupenda kama Haujawahi kulia Kuna muda mtu mbaya Hutengwa na hatia Maana kafiri hazaliwi Utengenezwa na dunia Ukijiua sitakuona Mzembe amini Nitakuvalisha pete Ruksa uipeleke baharini Najua tiba ya Upweke amini Mwisho wako ni Kuwa kicheche kama Mimi Hapo utajua kunihukumu Sio haki Mwanamke kama Wewe ndio amenifanya Niwe muasi Bila hofu wala Kiwewe Nitaendelea kuzunguka Kutafuta wasichana Vipofu kama wewe Sina hatia
Writer(s): Edger Vicent Mwaipeta Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out