Lyrics

Nakurupuka kitandani baada ya ndoto za kutisha Moyo unadunda sana na jasho linanitiririka Macho nafikicha, taswira, naona kiza Kwa muda nasizi kimya na dakika zinapita Zikijirudia ndoto hatari naona woga Nakosa hoja napotafakari nilichoota Namwamsha wife aniwekee maji ya kuoga Ananijibu anahisi homa na mwili mzima umechoka Nampa pole, Staki kuanzisha zogo wala nini Maana hata sura inaonesha ana kinyongo na mimi Ni muda sasa napokua nae hajiamini Nacheki saa nagundua nimechelewa kazini Napiga zangu maji mwilini And just for the record, Mimi ndo mtunza funguo za ofisini Nakuta wafanyakazi na bosi wapo getini Kwa ghadhabu kila mmoja akinitazama mimi Kabla sijameza mate wala sijabuni sala Naambiwa walikuja wazabuni kwa biashara Na kwakua nilichelewa kufungua ofisi Mchongo ukafa, nimeingizia kampuni hasara Baada ya masaa kibao ya kufikiri Ofisi ikaweka kikao kunijadili Waliniona driver nimeangusha basi Wakafikia mwafaka wakunifukuza kazi Nikatahamaki, sikujua lakufanya Pale kwenye kamati hakuna wa kumtazama Nikahisi ni mipango ya kikuda imefanywa Sio gari tu, maana hata nyumba nilinyang'anywa Nikajiuliza huruma imekwenda wapi? Kila mtu alijua kua nilipenda kazi Niliheshimu kama navyoheshimu ndoa ama mzazi Ama muumba, leo nimepata doa kwenye shati Acha familia, vipi deni la ofisi Wamenipa mwezi, nikifeli watanifilisi Mtoto shule, pia bunju nina shamba la kukopa Sijalipa na kijiji nina ndugu wa kutosha Nguvu zilimalizika, nikatoka kwa adabu Licha ya ghadhabu kunishika Nikajipa moyo kua nna mikono pia na miguu Vyote vyangu sina sababu ya kushindwa Nilikosa wa kunishika wa kumweleza Mshahara ulikua mdogo nilishindwa kuwekeza Nikapiga moyo konde mimi mwanaume nita-fight Nikpanda gari nikampe taarifa wife Nikiwa ndani ya dimbwi la mawazo Nikitafakari hivi vitimbi na vikwazo Mbele yangu akakatiza mpita njia Kwakua sikua makini na gari nikamvamia Dakika mbili, wananchi wakalizunguka gari Wakinishutumu sana sababu ya mwendo mkali Nikaitikia wito nikitegemea thawabu Nikampeleka mgonjwa na akaanza matibabu Narudi zangu home, misemo ya kishenzi nikitema Chumbani nasikia mihemo ya mapenzi Bila hodi, mlango nikaufungua kwa ghadhabu Nikamkuta house-boy juu ya kifua cha mke wangu! Nikabaki kama zuzu Yule wa kunifariji ndio ameniletea uchungu Nilitaka nilianzishe sikua na nguvu Huku nafsi inanishauri kwamba nimwachie Mungu Swalini kwamba sina moyo mkunjufu? Au kwakua muda sijaenda kuabudu? Au tuseme mja nina gundu? Au kwakua nilijenga nyumba na sikuwajulisha ndugu? Sijaona faida ya pato langu Wazazi walikufa bila kula jasho langu Mawazo kwenye kichwa yamezidi Dunia ina watu wengi na sioni wa kunifariji Naitazama ardhi, naitazama mbingu Sioni nuru nachoona ni maumivu Maswali mengi, bila majibu Ila Swali kubwa ni vipi mimi nitaimaliza siku? Jua linazama bado sijiamini Naona nadondoka ila sioni nikifika chini Saa tano na dakika hamsini Bado dakika kumi siku iishe na sijui kinafata nini Oh my God
Writer(s): Edger Vicent Mwaipeta Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out