Music Video

Music Video

Credits

PERFORMING ARTISTS
Ambwene Mwasongwe
Ambwene Mwasongwe
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Ambwene Mwasongwe
Ambwene Mwasongwe
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Thimos Chelula
Thimos Chelula
Producer

Lyrics

[Verse 1]
Ilitokea hawakupenda ndio mzunguko wa maisha
Na kama lingekuwa fungu, wasingechagua
Wanahangaika wanateseka
Wanapata shida hawana tumaini
Wameshaachwa wako peke yao
Mungu watazame kama Baba yao
Wanakutegemea wewe
Wanakutazama Bwana
[Verse 2]
Kilio wanacholia wanalilia moyoni
Maana hata wakilia nani atawafariji
Mungu uwasaidie uwatie moyo
Mzigo uwe mwepesi
Mzigo uwe mwepesi
[Verse 3]
Jamii imewasahau wanahangaika
Hata wakiombaomba wanawafukuza
Wengine wanawatukana kuwaita chokoraa
Mungu uwakumbuke
Mungu uwakumbuke
[Chorus]
Wakiachwa peke yao ubaki nao
Kaa pamoja nao kwenye baridi kali
Kavifunge vidonda vya mioyo yao
Kazibe pengo lililo mioyoni mwao
Wakumbushe wewe ni Baba na Mama yao
Wakumbushe wewe ni Baba na Mama yao
[Bridge]
Ayayayah una macho huoni na hata ukiona huoni umuhimu
[Verse 4]
Jifanye kama umekufa uko kuzimuu
Sasa inua macho yako tazama duniani
Watazame wanao wanavyoteseka
Wanadhurumiwa
Wananyanyasika
[Verse 5]
Sasa nyosha mkono wako, uwape chakula
Nenda kawatafutie vya kujifunikaa
Unagundua hauwezi maana hauna mwili
Tena hawakuoni
Maana ulishakufa
[Verse 6]
Sasa unawafanya nini watoto wa marehemu
Mbona unawadhurumu mali za wazazi waoo
Sivyo walivyokuachia ili uwanyanyasee
Usiwatende ubaya
Ili usije kutendewa
[Verse 7]
Hivi una uhakika gani kama ukiondoka
Utamwachia nani watoto wakoo
Je! Wakija kuwatenda kama utendavyo wewe
Utajisikiaje?
Je! Hayo utayapenda?
[Chorus]
Wakiachwa peke yao ubaki nao
Kaa pamoja nao kwenye baridi kali
Kavifunge vidonda vya mioyo yao
Kazibe pengo lililo mioyoni mwao
Wakumbushe wewe ni Baba na Mama yao
Wakumbushe wewe ni Baba na Mama yao
[Bridge]
Ayayayayyaah
Hali zao ni mbaya
[Verse 8]
Tazama walivyopauka wa kwako wanatakata
Tena watupa chakula wao hawana
Wanatamani Baba angekuwepo
Mama angekuwepo wasingepata shida
Hawaelewi nini kimewatokea
Wanjiona wana mikosi jamii imewasahau
Tuwahurumieni hawa
Tuwaonyeshe upendo wetu
[Verse 9]
Wengine kwa kujitetea wakaangukia pabaya
Wamefuata mikumbo wako pabaya
Wengine wametenganishwa na wadogo zao
Wengine wako jela lakini tatizo ni nini?
Walijaribu kuokoa maisha yao
Wakaenda kuiba
Wengine wanachomwa moto
Tunawalaumu bado
Kumbe tatizo tumewasahau
[Verse 10]
Wananenewa maneno makali
Wanasimangwa hadi wanauguaa
Ila wafanyaje wanajikaza
Hawana pa kwenda wanavumilia
Mungu ingilia katii
Written by: Ambwene Mwasongwe
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...