Music Video
Music Video
Credits
PERFORMING ARTISTS
Ambwene Mwasongwe
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Ambwene Mwasongwe
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Thimos Chelula
Producer
Lyrics
[Verse 1]
Ninamkumbuka mama mmoja
Aliyekuwa na watoto saba
Alikuwa akimcha Mungu
Akimwomba mchana na usiku
[Verse 2]
Ulipita muda sijaonana naye
Nikaamua niende nimtembelee
Nikamkuta mama mjane amechoka
Macho yamevimba kwa kulia
[Verse 3]
Akanitazama akaniambia
Ajali imeua watoto wangu
Tazama kaburi kama matuta
Mungu hakunisazia kitu
[Verse 4]
Akanikumbusha unajua mwanangu
Wewe Bado ni kijana mdogo
Usijefikiri kumwacha Mungu
Hata kama amekuumiza
Akapiga magoti akitetemeka
Akamuomba Mungu mbele yangu akisema
[Chorus]
Kwanini uliamua kuchukua wangu tu
Mtaa mzima hukuona wengine
Kwanini ajali moja iliuwa wangu tu
Kwa nini siku moja walizikwa wangu tu
[Chorus]
Kwanini hukuamua hapa mtaani
Angalau kila nyumba angekufa mmojammoja
Hata nijiulize maswali mengi
Jibu bado litabaki wewe ni Mungu tu
Najua uliniamini hili naliweza
Hivyo basi nasema jina lako libarikiwe ameen
[Verse 5]
Kama kawaida wanadamu
Wakanyanyua vinywa wakasema
Kila mmoja alioongea lake
Ili mradi wamvunje moyo
[Verse 6]
Wapo walojifanya kuwa wana uchungu
Kumbe moyoni wanamng'ong'a
Wengine wakadiriki kusema hadharani
Alijivuna sasa kiko wapi
[Verse 7]
Mama anasema akiwa msibani
Alihisi mwili unawaka moto
Aliona kaka Mungu hayupo
Dunia yote kaachwa peke yake
[Verse 8]
Waliomfariji aliwaona waongo
Hawajui uchungu wa msiba
Huzuni ilipozidi akalia sana
Asikubali kufarijiwa
[Verse 9]
Ghafla akakumbuka mtetezi wake
Kwamba Mungu wake yuko hai
Akishampitisha kwenye tanuru
Mwisho atang'ara kama dhahabu
[Chorus]
Ulipomchukua mume wangu Bwana
Watoto walinifariji
Sasa umeamua kuwachukua wote
Hukunisazia kitu
[Chorus]
Umenibebesha mzigo mzito sana
Siuwezi peke yangu
Bila msaada wako sitaweza mimi
Naomba nisaidie eeh
[Verse 10]
Kama unadhani la kwako zito
Basi sasa jifunze kwa wenzako
Maana wewe kuguswa tu na tatizo
Unanung'unika mwaka mzima
[Verse 11]
Waweza kudhani kwamba unaumwa
Kumbe hujaona wagonjwa
Ukishawaona wagonjwa wenyewe
Unaweza kupona bila dawa
[Verse 12]
Mungu anao watu anaowaamini
Watu wenye misuli ya imani
Wao wanapopita kwenye magumu
Wanamtukuza katika hayo
[Verse 13]
Hawa ndio watu Mungu huwatumia
Kumsimangia shetani
Maana kujaribiwa kwa Imani zao
Huleta utukufu kwa Mungu
[Verse 14]
Mama anasema Mungu ni mwema
Kwa sababu amenitetea
Katika kupita kwenye magumu
Nimeona mkono wa neema
[Chorus]
Ashukuriwe Mungu wa watakatifu
Anayetupa kushinda
Hata tukipita kwenye magumu gani
Hatatuacha peke yetu
Ametuahidi atakuwa nasi
Ukamilifu wa dahali Ameen
Written by: Ambwene Mwasongwe


