Music Video
Music Video
Credits
PERFORMING ARTISTS
Monaja
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Mwongela Kamencu
Songwriter
Kevin Gachuma Waithaka
Songwriter
Lyrics
Manze acheni kutubeba wana nasi watu wazima, sisi watu wazima
Changamkeni mlitupa ahadi basi nyinyi timiza, nyinyi timiza
Mnatutoshanisha, toshanisha (Ishatosha!) toshanisha, toshanisha (Ishatosha!)
Mnatutoshanisha, toshanisha, (Ishatosha!) toshanisha, toshanisha (Ishatosha!)
(Monaja) Naitwa naja, youth leader wa chama tawala, tumemuok mashinani kufungua tawi la chama
Muriega? (yeh turiega), Kutakuwa na lami na power juu gava ni yetu mtajua haki usawa
(Man Njoro) Uh.. herro brother kabra urete hiyo mada niko na mswala kwanza
kabra ulete hiyo mswada umekuja na mkwanja? ra sivyo ka masaa
Mavijana wako njaa hebu toa kitu mani sir..
(Monaja) Acha tamaa za saa hii saa hii fikiria kesho na kutwa
Wee ni kijana ka me panletta mchezo kwa future
Mtu wetu alishinda maze heko mtatupa
Hii si ushindi tu ya chama hebu weh ngoja muda
(Man Njoro) Ushindi nyi ndio mlipata si tunajikaza kisabuni
Mlituahidi tuna share kumbe nyi ndio wenye kampuni
Siku ya kura mlitusihi “amkeni nduguzanguni,”
Mkapata kiti lakini sisi maisha duni
Manze acheni kutubeba wana nasi watu wazima, sisi watu wazima
Changamkeni mlitupa ahadi basi nyinyi timiza, nyinyi timiza
Mnatutoshanisha, toshanisha (Ishatosha!) toshanisha, toshanisha (Ishatosha!)
Mnatutoshanisha, toshanisha, (Ishatosha!) toshanisha, toshanisha (Ishatosha!)
(Monaja) Me na weh tuko pamoja, Buda kuwa mpole
Si tuliandika mmoja wetu? anaitwa Njoroge
‘Sikae mbali na kivuli jua lisikuchome
Kushinda kwa mmoja wetu ni kismat kwa wote..
(Man Njoro) Bahati gani? time ya campaign mlisema ati hatutaumia
Ati si watoto wa Mau Mau mashamba mtatupatia
Mkaingia mkaongeza tax sa mkatugeuzia
Mnafuata tu kile mnaambiwa na bank ya dunia!
(Monaja) Bank ya dunia ni wafadhili tungekuwa wapi bila wao,
Kumbuka mlami alikam na stima tumshukuru kila uchao
Hata hao wanalipa tax ndio wameendelea kule kwao,
So tukiwaongezea huku hatuelewi mshangao
(Man Njoro) Unga na shugey imepanda ninasumbuliwa na missis,
Kuna Baraka kwa hizo shida hutapata diabetes
(Man Njoro) Pia hamsini haifiki town natokea ngara siku hizi
Ni mazoezi unapiga itasaidia kujenga mwili!
Manze acheni kutubeba wana nasi watu wazima, sisi watu wazima,
Changamkeni (twi andu agima)mlitupa ahadi basi nyinyi timiza(tamere sir), nyinyi timiza
Mnatutoshanisha (tosha tosha), toshanisha (Ishatosha!) (tosha tosha), toshanisha, toshanisha (Ishatosha!)
Mnatutoshanisha(tosha tosha), toshanisha, (Ishatosha!) (tosha tosha),toshanisha, toshanisha (Ishatosha!
(Man Njoro) Lakini enyewe nyi wasee mlikuwa mnatuenjoy
Kutupamba roho na hurubarrow sasa ni maconvoy
Kazi matour za dunia kama Vasco wa Da Gama
Pesa ya mafuta ya kupika mlitupima na mkazama
Mnatukula mkituliza mnatuuma mkipuliza
Kisha pesa ya kanisa mnasupport na miujiza
Hizo ndoto za mchana mnatuchoresha na giza
Mnatuingiza nyuki kwa mdomo mnatushow si tukimye
(Monaja) Wheelbarrow? Ah hiyo ilikuwa lugha ya biashara
Hata konkodi hudai kirai imebaki wawili kujaza
Kijana kujitetea kwa denge hutumia lugha kumbamba
lakini si tukifanya the same tunakuwa wabaya
Nchi saa hii inapitia shida tunafaa kuombewa
So wachungaji wakitusupport mnafaa kuelewa
Hii maandamano unaona tu ni ya kuchochewa (ati)
(Monaja) Kenya ni nchi ya amani wakubwa wanafaa kuombewa
(Man Njoro) Sa kijana ako nyumbani amekosa kazi akona amani?
(Monaja) Kenya ni nchi ya amani inafaa kuombewa,
(Man Njoro) Aiiiii…Na wale wamelala njaa bila kitu sahani wana amani?
(Monaja) Kenya ni nchi ya amani inafaa kuombewa
(Man Njoro) Acha hizo…Na wale wagonjwa hawana madawa wamelazwa hospitali?
Kenya ni nchi ya amani inafaa kuombewa
(Man Njoro) Aiiiii Onanikii dirakuuria sir? mbona nakuuliza hizi maswali
(Monaja) Kenya…eh amani inafaa kuombewa
Manze acheni kutubeba wana nasi watu wazima, sisi watu wazima,
Changamkeni (twi andu agima)mlitupa ahadi basi nyinyi timiza(tamere sir), nyinyi timiza
Mnatutoshanisha (tosha tosha), toshanisha (Ishatosha!) (tosha tosha), toshanisha, toshanisha (Ishatosha!)
Mnatutoshanisha(tosha tosha), toshanisha, (Ishatosha!) (tosha tosha),toshanisha, toshanisha (Ishatosha!)
Written by: Kevin Gachuma Waithaka, Mwongela Kamencu