album cover
Usinipite
9,921
Christian & Gospel
Usinipite was released on April 18, 2025 by Walter Chilambo as a part of the album Destiny Helper - Single
album cover
Release DateApril 18, 2025
LabelWalter Chilambo
Melodicness
Acousticness
Valence
Danceability
Energy
BPM66

Music Video

Music Video

Credits

PERFORMING ARTISTS
Walter Chilambo
Walter Chilambo
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Walter Chilambo
Walter Chilambo
Songwriter

Lyrics

(Love music)
Ee Bwana nainamisha kichwa changu (ninakuabudu we)
Na tena nainua mikono yangu (kukuadhimisha we)
Na ninashuka kwa unyenyekevu madhahabuni pako
Maana majibu ya maswali yangu
Baba nitapata kwako
Kwanza nahitaji rehema zako
Unisafishe Bwana
Kwa yale nayajua na nisoyajua
Niwe safi Bwana ninaomba neema yako
Na kibali chako juu yangu wee
Nitembee kifua mbele
Yesu unapozuru wengine (usinipite)
Nikumbuke (usinipite)
Maombi yangu (usinipite)
Baba uyakumbuke (ah, ah usinipite)
Nyakati za majaribu (usinipite)
Uniguse (usinipite)
Ingawa mi si mkamilifu (usinipite)
Nikumbuke (ah, ah usinipite)
Natamani nikuone
Yesu niguse vazi lako
Natamani niwe Batimayo
Unifumbue macho
Unifundishe maana we mwalimu wa imani
Nitapita salama
Maana akili zangu zimefika mwisho
Tumaini lipo kwako Bwana
Na unijaze roho wako mtakatifu
Ashike fahamu zangu
Nihisi niki kulingana nawe Bwana
Maana wajua ninayoyapitia
Nahitaji huruma yako
Ee Mungu kadiri ya fadhili zako
Usinipite
Ninaomba eh (ninaomba neema yako)
Zaidi nisimame nitangaze
Uzuri wako Bwana
Yesu unapozuru wengine (usinipite)
Nikumbuke (usinipite)
Maombi yangu (usinipite)
Baba uyakumbuke (ah, ah usinipite)
Nyakati za majaribu (usinipite)
Uniguse (usinipite)
Ingawa mi si mkamilifu (usinipite)
Unikumbuke (ah, ah usinipite)
Maana hakuna nguvu ipitayo jina lako (usinipite)
Ni we unaweza (usinipite)
Navunja maagano yote (usinipite)
Nikumbuke (ah, ah usinipite)
Adui ni mkali (usinipite)
We Yesu nakuomba (usinipite)
Ninapokosa tumaini (usinipite)
Unikumbuke (ah, ah usinipite)
Walter
Written by: Walter Chilambo
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...