album cover
Njoo
2,053
Music
Njoo was released on August 13, 2004 by Sony Music Entertainment East Africa as a part of the album Safari
album cover
AlbumSafari
Release DateAugust 13, 2004
LabelSony Music Entertainment East Africa
Melodicness
Acousticness
Valence
Danceability
Energy
BPM100

Music Video

Music Video

Credits

PERFORMING ARTISTS
Ferooz
Ferooz
Performer
COMPOSITION & LYRICS
Feruzi Mrisho Rehani
Feruzi Mrisho Rehani
Lyrics
PRODUCTION & ENGINEERING
P-Funk Majani
P-Funk Majani
Producer

Lyrics

Oh yeah
Nisikie nnachosema
Lawama toka kwa daz wanalalama shemeji yao mbona umewatelekeza
*** nao wanashangaa mbona ghafla umeniacha kwenye giza
Mpaka sasa sijagundua wapi moyo wangu nitaenda kutua
We ndio wangu pumziko, sasa mbona waniacha kwenyemafuriko
We niwangu pumziko, sasa mbona waniacha kwenye mafuriko
Tulisha weka nadhiri na kuapa mbele ya bwana milele hatutoachana
Mashuhuda wetu walikua malaika wa bwana sasa mbona leo unanikana
Mwisho wa safari haujafika ghafla moyoni mwangu umeadimika
Bara visiwani mbuga na nyika nakutafuta labda nitafarijika
Mashariki magharibi kasi na kusi nakutafuta bado tu umeadimika
Nafsi inafadhaika inataabika rudi kwangu bado unahitajika
Njoo uniokoe kwenye garika mauti yatanifika mwishoe nikose wakunizika
Njoo, njoo, mpenzi njoo
Mbona unaniruka mbona unaniruka
Acha kunigeuka laazizi
Mbona unaniruka mbona unaniruka
Acha kunigeuka mpenzi
Ona wanasema sana njoo eti tumefarakana
Ona wanasema sana eti tumefarakana
( njoo )
What gwan, rude bway rude bwaaay
Eti wanakushauri kwamba me sifai
Na ukirudi kwangu utapata kizai zai
Kila wakidamkapo wanawahi kusambaza unafki
Wanasahau ata kunywa chai
Achana nao wanafki walio kosa hoja
Wanachongoja ni si kutokuwa pamoja
Wanaleta vioja
Njoo tuwe pamoja tuanze kujikongoja
Daz ndo kwa ma soldier soldier kwanza ngoja
Sitoacha kuimba
Sitoacha kwasababu moyo wangu mimi mwenzako unashindwa kuvumilia
Kila nikilala nateseka naweweseka kwaajili yako fanya kunihurumia
Ni vigumu kuamini kama leo bega langu la pili umenikimbia
Maswali mengi najiuliza ni kitu gani mpenzi wangu kilichokukimbiza
Au labda ufukara wangu moyoni mwako ulikua unakuchukiza
Mapenzi uvumilivu uaminifu pamoja na kukumbana na vikwazo uwe tayari
Nasi tumetoka mbali kwenye safari tumevuka mito maziwa na bahari
Leo umeniacha pekeyangu nateketea jangwani mpenzi hilo hata we hujali
Mpenzi rudi nyumbani mwenzako mi umeniacha gizani njoo
Njoo mpenzi sina tofauti na ndege aliokatwa mbawa ghafla siwezi paa angani
Njoo mpenzi kama nimekosa nisamehe tafadhali mpenzi rudi nyumbani
Njoo mpenzi ukiniacha utakatili nafsi yangu usababishe mi nihame duniani
Njoo mpenzi sikia hata Majani anatumia vyombo kukubembeleza honey
Njoo
Mbona unaniruka mbona unaniruka
Acha kunigeuka laazizi
Mbonaunaniruka mbona unaniruka
Acha kunigeuka mpenzi
Ona wanasema sana njoo eti tumefarakana
Ona wanasema sana eti tumefarakana
( njoo )
Written by: Feruzi Mrisho Rehani, Paul Peter Matthijsse
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...