album cover
Lissa 3
4,371
Hip-Hop/Rap
Lissa 3 was released on September 30, 2025 by Wanangu99 as a part of the album Lissa 3 - Single
album cover
Release DateSeptember 30, 2025
LabelWanangu99
LanguageEnglish
Melodicness
Acousticness
Valence
Danceability
Energy
BPM90

Credits

PERFORMING ARTISTS
Rapcha
Rapcha
Performer
Cosmas Paul Mfoy
Cosmas Paul Mfoy
Vocals
COMPOSITION & LYRICS
Cosmas Paul Mfoy
Cosmas Paul Mfoy
Songwriter
PRODUCTION & ENGINEERING
Gachi B
Gachi B
Producer

Lyrics

Just like a miracle
Nafumbua macho niko ndani ya kuta nne
naona mtu mkononi ameshika stethoscope
Niko chali kama panya maabara
Na ndo hapo nikagundua niko hospital
Kando kuna doctor amesimama
Alienihudumia kwa miezi kama 9 niliyolala kwenye COMA
Akishuhudia umati uliokuja kuniona hospitali ukipungua wakiamini sitopona
Wakuabudiwa ni Mungu tu
Akisimama yeye amimi hakuna kiumbe wa kumpandishia kibesi juu
Nguvu zote anazo yeye
Mwanadamu hawezi gusa roho ya mtu labda atauchubua mwili tu
Okay, masaa yakapita
Nikaruhusiwa kurudi nyumbani na nafuu nkawa nshaipata
Mama alirejesha tabasamu ambalo alipoteza muda mrefu tangu siku msala umenipata
A week later
 
Mawazo ndo yakaanza nizidia
Muda nliopoteza unanistress na naumia
Nkahisi nimeharibu vyote shule na career
Wazo la kisasi kichwani linanirudia
Nikaongea na Majani akanambia
Inabidi uje Arusha upate muda wa kutulia
Hiki kipindi ambacho unarecover isingefaa ukakaa mwenyewe bora ukae na familia
Ikafika siku ya safari
Najiandaa nasafari,
Naskia mlango unagongwa harufu nzuri kwa mbali
Hii perfume naijua, lissa aliwahi kuitumia mara chache ikanikumbusha mbali
Moyo ukaanza kukimbia mbio
Nkaamini kweli mwisho wa tukio mwanzo wa tukio
Nkajikaza kiume nkaenda kufungua
Alikua room mate wa Lissa hostel nikamtabua
Akaingia then tukaanza kuongea
Akanambia pole sana kwa maradhi na yaliyotokea
Akasema leo alipita hospitali wakamwambia mgonjwa amepata nafuu home amesharejea
Basi Nkamuuliza vipi kuhusu lissa
Akanipa mkasa mzima baada ya kile kisa
Akaniambia kuwa alitemwa na bwanaake baada tu ya kushika mimba
Na mguu wa chuo alikata kabisa
Afu pia askari upelelezi wanamfatilia
Kila anapotia mguu askari wataingia
Miezi kama 9 hajaonekana amepotea kabisa na hawajui wapi amekimbilia
Nkamwambia okay thanks my dear
Leo nna safari na muda wa kuondoka naona umekaribia
Nkamuachia namba ya simu akaondoka
Haikupita muda sana na mi nikaondoka
So, Nika-fly mpaka Arusha nikatua
Mwanangu wala hakuchelewa akaja airport kunichukua
But before twende home
Akasema tupite super market kuna vitu anataka chukua
Sa tukaenda kununua
Nkiwa super market nanyanyua uso nkaona mtu nnae mjua
Ye aliponiona akaanguka kwa mshtuko
Nikaharakisha kwenda kumnyanyua
Alikuwa best yake na lissa
Walisoma wote high school chuo tu wakatenganishwa
Nkaenda nae mpaka nje na mahemezi yakasimamishwa
Hakuamini kuniona kabisa
Akaniuliza hivi unajua lissa alipo!?
Nkamwambia sihitaji hata kujua alipo
Akanisihi nitumie hekima nimpe ata dakika
Anipe hata kwa ufupi story tu ilivyo
Akasema lissa ana hali mbaya
Akili kama imemruka baada ya mawazo kumsonga vibaya
Kateseka na mimba miezi 9 yuko hoi
Leo kajifungua na mtoto ni wako mfoy
Mie mdomo wazi
Mwili wote ganzi
Uku macho yamenitoka ka nakataroho juu ya kitanzi
Akaniambia lissa alimuahikikishia
Na alijua kua anamimba wiki ya pili baada ya mimi kumfumania
Sikuwa na la kubisha
Mapenzi yangu kwa lissa yalirudi kama mwanzo baada ya ile taarifa
Tukaongozana tukaondoka mpaka hospitali
Tukaruhusiwa kuonana na lissa
mapigo ya moyo kasi yananipiga
Nkamuona lissa kitandani, mwili wake umedhoofika
Ye aliponiona akapatwa na mshtuko kama shoti imepiga
Uku na machozi yanatiririka
Nkasogea nikamchukua mtoto,
nlidata, maskio mpaka mdomo amekosa tu rasta
Nkaambiwa muda wote mtoto alikua analia
Ila amenyamaza pale tu ulipompakata
Nkamgeukia mamaake nkiwa naskia uchungu
Nkamwambia Lissa ni nini hasa ulichokipata!??
Tungeishi kwenye ahadi zetu tungeweza timiza ndoto zetu na vile vyote ulivyotaka tungevipata
Muda wote lissa ananiangalia
Bila kupepesa macho wala kuniitikia
Kumbe Ule muda nilipotia mguu ndani ya hicho chumba
Kwa Mshtuko aliopata aliaga dunia
Kwenye kitabu cha majina ya wanadam waliowahi kupenda jina langu naomba msiache kuliandika
Ubavu wa kushoto umedanganywa na nyoka
Kisa fasheni
Ameniachia mtoto wa kike nimempa jina Eden
Written by: Cosmas Paul Mfoy
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...