Listen to Muhogo Wa Jang'ombe by Bi Kidude

Muhogo Wa Jang'ombe

Bi Kidude

World

1,946 Shazams

Lyrics

Muhogo wa Jang'ombe, sijauramba mwiko Usitukane wakunga, na uzazi ungaliko Kaditamati naapa, muhogo sitonunua Haikuwa Maimuna, aliyekwenda ung'oa Kapata tete kuanga, na ugonjwa wa shurua Kula dori kula dori, mshindo wa sufuria Guliguli guliguli, kofia ina viua Ndiye mimi ndiye mimi, anipataye ukoa Mungu akitaka kupa, hakuletei barua Hukupa usingizini, pasi mwenyewe kujua Kwenda mbio sikupata, bure unajisumbua Mkato wake matege, wakati anapokuja Naliiweka dhamiri, ya kumfulia koja Wallahi nimeghairi, kiumbe hana mmoja Kamfunge kamfunge, beberu wa Athumani Umfunge umfunge, pahala panapo jani Endaye tezi na omo, atarejea ngamani Sina ngoa sina ngoa, kuhadaiwa sitaki Ni mwerevu ni mwerevu, wala sihadaiki Pambanua pambanua, viwili havipendeki Ya nini kutakadamu, kwa jambo lisilokuwa Utahadhari na mwiko, wakati wa kupakua Ukitamani makoko, chungu utakitoboa Nauliza masuala, hamnambii jamani Watu wake wakishiba, huzidi umaluuni Pahala pasipo ngoma, hupandwaje na shetani Nyimbo ya Bi Kidude Imeletwa na Hassan O. Ali
Writer(s): Kidude Baraka Bi, M Ilyas Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out