album cover
Mama
album cover
Mama was released on July 8, 2026 by Kassam Music as a part of the album Mama - Single
July 8, 2026
LabelKassam Music
BPM120
Melodicness
Acousticness
Valence
Danceability
Energy

Lyrics

Kassam leo namuimbia mama
Unaitwa na mama,
Una vuta mdomo.
Unatumwa dukani,
Unaweka mgomo.
Wenzako hiyo nafasi wanaitamani,
Maana wazazi wao hawapo duniani.
Wiki nzima upo kimya, humpigii hata simu,
Halafu unampost unampenda, huo si uwazimu?
Mwenyewe amekusomesha kwenye hali ngumu,
Halafu shida zake leo unaziona kama sumu.
Nimemmiss sana mi ndio maana nalia,
Nimemkumbuka mama my dear.
Mtunze sana mama, hiyo ndio pepo ya dunia,
Maana hatorudi tena akisha potea.
Mpende mama yako sasa,
Sio mpaka afe ndo useme unampenda.
Mpende mama yako sasa,
Sio mpaka afe ndo useme unampenda.
Nimemmiss sana mi ndio maana nalia,
Nimemkumbuka mama my dear.
Mtunze sana mama, hiyo ndio pepo ya dunia,
Maana hatorudi tena akisha potea.
Mpende mama yako sasa,
Sio mpaka afe ndo useme unampenda.
Mpende mama yako sasa,
Sio mpaka afe ndo useme unampenda.
Kutwa wachezea pesa club na hauwazi,
Unapambwa na machawa tajiri, ukifa eti hauozi.
Mama hata hela ya chai hana, hata hiyo mia ya mandazi,
Sasa tuseme amepata mtoto ama amepata bazazi?
Hakuna kitu kinachomuuma mzazi,
Kama azae mtoto halafu akue nje ya malezi.
Aaah, nawe tambua utakuwa mzazi,
Unachomfanyia mama yako utafanyiwa na chako kizazi.
Aaaaah eeeeee...
Mpende mama yako sasa,
Sio mpaka afe ndo useme unampenda.
Mpende mama yako sasa,
Sio mpaka afe ndo useme unampenda.
Mi nampenda mama yangu,
Na wewe mpende mama ako.
Written by: Kassim Rashidi Abed
instagramSharePathic_arrow_out􀆄 copy􀐅􀋲

Loading...