Lyrics

Nirahisi kinywa kujawa na lawama tele Pale mambo yanapoonekana hayaendiii Ni ajabu sana namna moyo unahangaika (kutafuta majibu) Ajabu sana moyo unavyoonyesha mashaka yakwamba japokuwa Mungu anaishi ndani yangu kuna muda nahofu, japokua Mungu anaketi kati yetu kuna muda nahofu, Ahh nakumbuka wana wa Israel katika bahari yashamu japo walikatiza katikati ya bahari kwa ushindi, Kwa nyimbo nyingi waliimba na kumsifu Bwanaa. Lakini baada ya kuvuka na kuliona jagwa yalibadilika mambo, Manung'unikoo yalisimama na kusahau muujiza alotenda Bwana Mwanzo aah. Eee MUNGU Niisaidieee eee eenhee BRIDGE -Nikumbushe wema wako nisije laumu Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machoziii, x2 Eeeh Ee MUNGU Nisaidiee Nisaidieee kukumbuka baba yakwamba umenichora kiganjani mwako kati ya wengi walioko duniani eenh na mimi umenionaa oooh ooo Nikumbushe baba yakwamba ni wewe umeniponya nilipoumwa yakwamba ni wewe mlipaji wa ada yangu shuleniii. ouoooh ooh Yakwamba kama ungeniacha hatua moja nisingelifika nilipo ooh eee Babaa umenikung'uta mavumbi, kung'uta mavumbi mimi na kuniheshimisha. Oooooh oooooh Nikumbushe wema wako nisije laumu Nikumbushe ukuu wako wakati wa Magumu(Nisaidie Yesu) Nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu Niimbe wimbo wa sifa katikati ya machozii ×2
Writer(s): Angel Benard Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out