歌词

Bwana Yesu nakupenda, wewe uliyenipenda mimi Sina chochote cha kulipa chalingana na upendo wako Ya thamani yote ni yako Ata hivyo yasingeweza kulipa Uliotenda ni makuu sana mimi siwezi kueleza Yanishangaza, yanipita je niseme nini, bwana wangu Mwanadamu nisiyestahili Kunipenda ata kunifia, eh bwana Bwana wetu, eeh Mungu wetu Twasimama mbele zako bwana Tumekujaa kukushukuru bwana Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana) Bwana wetu, eeh Mungu wetu Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa) Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu) Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana) Ungeweza kutojali mwanadamu akaangamia Kwa kuwa yeye ndiye aliitenda dhambi sio wewe bwana Ungeweza kumuumba mwengine Mwenye dhambi, usimkumbuke tena Lakini kinachoshangaza maamuzi yako ni kinyume Uliamua kumpenda yule-yule ambaye apendeki Eeh bwana tuseme nini Pendo lako limetuzidi, eh bwana Bwana wetu, eeh Mungu wetu Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa) Tumekujaa kukushukuru bwana Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana) Bwana wetu, eeh Mungu wetu Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa) Tumekujaa kukushukuru bwana Na kukusifu usifiwe milele Ndugu yangu fikiria sana pendo hili la thamani Tutapata je kupona tusipolijali pendo hilo Kila jambo limewekwa wazi Karibia msalaba wake Ebu njooni twende kwake tuzitubu dhambi zetu zote Hatuna muda tena ndugu, pendo hili lisipite bure Ni salama mikononi mwake Mtetezi tena ushindi wetu (eh bwana) Bwana wetu, eeh Mungu wetu Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa) Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu) Na kukusifu usifiwe milele (eh bwana, eh bwana, eh bwana) Bwana wetu, eeh Mungu wetu Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa) Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu) Na kukusifu usifiwe milele (ewe bwana) Bwana wetu, eeh Mungu wetu (ewe bwana) Twasimama mbele zako bwana (tumekujaa) Tumekujaa kukushukuru bwana (na kukusifu) Na kukusifu usifiwe milele
Writer(s): Ambassadors Of Christ Choir Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out