歌詞

[Verse 1]
Nabii Eliya, aliwaita manabii wote, wa mungu baali
Nabii Eliya, aliwaita manabii wote, wa mungu baali
Lengo la Eliya, ilikuwa ni kumthibitisha Mungu wa kweli ni yupi
Kati ya Mungu wa baali, na Mungu wa mbinguni
Eliya, Eliya
[Verse 2]
Akawambia watu nikaribieni mimi, akachukua mawe kumi na mbili akaanza kujenga madhabau
Akaweka kuni juu yake, akaweka sadaka juu yake
Akachimba mfereji, akawambia watu mwageni maji mapipa manne
Wakamwaga maji mara ya kwanza, wakamwaga maji mara ya pili, wakamwaga maji mara ya tatu
Elijah, akaanza kumuita Mungu, Mungu wa mbinguni
[Chorus]
Wewe Mungu, wewe Mungu
Mungu wa mbinguni naijulikane kuwa upo
Wewe Mungu, wewe Mungu
Mungu wa mbinguni naijulikane kuwa upo
[Verse 3]
Moto ukashuka, ukaramba ile sadaka
Ukaramba zile kuni, ukaramba na yale mawe
Ukaramba na yale mavuno, ukaramba na yale maji
Watu wakasujudu, wakasema huyu ndiye Mungu
Anayepaswa kuabudiwa, ndiye Mungu ninaye mwimbia
Mungu wa Elijah oh oh oh
[Chorus]
Ooh Mungu (Mungu ni Mungu tu)
Ooh Mungu baba (Atabaki kuwa Mungu tu)
Huyu Mungu wa mbinguni jamani (Mungu ni Mungu tu)
Huyu Mungu wa Eliya (Atabaki kuwa Mungu tu)
Maishani mwako mama yangu wewe (Mungu ni Mungu tu)
Mahali pote unapotembea (Atabaki kuwa Mungu tu)
Ata wainuke wamseme vibaya (Mungu ni Mungu tu)
Ata wamkatae mbele yako (Atabaki kuwa Mungu tu)
[Verse 4]
Na wewe ndugu yangu, unayenisikia, unaye nitazama
Unaona nini mbele yako? Unaona nini mbele yako?
Pengine unaona majaribu haujui utafanya nini, we mkaribie Mungu tu
Pengine unaona magonjwa, haujui utapona lini we mkaribie Mungu tu
Pengine unaona vita kubwa, haujui utashinda vipi, we mkaribie Mungu tu
Pengine unaona watesi, haujui utapita vipi, we mkaribie Mungu tu
Pengine ni jaribu katika ndoa yako, haujui utashinda vipi, we mkaribie Mungu tu
Hakuna linaloshidikana kwake Mungu
Hakuna linaloshidikana kwake
Hakuna linaloshidikana kwake Mungu
Hakuna linaloshidikana kwake
Aliyemshindia Elijya katikati ya manabii wa baali
Atakushindia na wewe
[Chorus]
Ooh Mungu (Mungu ni Mungu tu)
Ooh Mungu baba (Atabaki kuwa Mungu tu)
Huyu Mungu wa mbinguni jamani (Mungu ni Mungu tu)
Huyu Mungu wa Eliya (Atabaki kuwa Mungu tu)
Maishani mwako mama yangu wewe (Mungu ni Mungu tu)
Mahali pote unapotembea (Atabaki kuwa Mungu tu)
Ata wainuke wamseme vibaya (Mungu ni Mungu tu)
Ata wamkatae mbele yako (Atabaki kuwa Mungu tu)
[Verse 5]
Wanadamu wamekusemea maneno, kwamba hautaweza, katika jaribu lako
Wanadamu wamekusemea maneno, kwamba hautashinda katika vita yako
Kumbe njia za Mungu, sio sawa na za mwanadamu
Njia za Mungu, sio sawa na za mwanadamu
Mipango ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu
Akili ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu
Maneno ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu
Mawazo ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu
Kazi ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu
Sauti ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu
Aliye mshindia Eliya
Atakushindia na wewe
[Chorus]
Ooh Mungu (Mungu ni Mungu tu)
Ooh Mungu baba (Atabaki kuwa Mungu tu)
Huyu Mungu wa mbinguni jamani (Mungu ni Mungu tu)
Huyu Mungu wa Elijah (Atabaki kuwa Mungu tu)
Maishani mwako mama yangu wewe (Mungu ni Mungu tu)
Mahali pote unapotembea (Atabaki kuwa Mungu tu)
Ata wainuke wamseme vibaya (Mungu ni Mungu tu)
Ata wamkatae mbele yako (Atabaki kuwa Mungu tu)
Written by: Christopher Mwahangila
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...