積分
演出藝人
Obby Alpha
演出者
詞曲
Obby Alpha
詞曲創作
歌詞
[Intro]
Yelele mama
Mmh yelele mama
Yelele mama
Mmh yelele mama
[Verse 1]
Hivi ni kweli kutakuwa na moto?
Maana sielewi kwa hizi changamoto
Hivi ni kweli kutakuwa na moto?
Maana sielewi kwa hizi changamoto
[Verse 2]
Hivi ni kweli mapenzi ya Mungu yameyazidi maombi yangu?
Maana ninachoomba sio knachokuwa
Hivi ni kweli mwizi anakuomba wewe?
Na mimi nikilala naomba nisiibiwe
[Verse 3]
Hivi unaona wengine wanatoa mimba?
Wakati wengine wanasaga meno kutafuta watoto
Hivi ni kweli inawezekana!
Baba mzazi akatembea na mwana
Hivi ni kweli inawezekana!
Mama mzazi akatembea na mwanae
[Verse 4]
Sijasema Bwana we ni kipofu
Ila naumia yamezidi maovu
Vipi ghadhabu yako we mwokovu
Ukija shuka nitaweka wapi sura Bwana
[Refrain]
Yelele mama
Mmh yelele mama
Yelele mama
Mmh yelele mama
Yelele mama
Mmh yelele mama
Yelele mama
Mmh mama
Yelele mama
Mmh yelele mama
[Verse 5]
Mungu nawaza ningekuwa wewe!
Yaani watu watumie jina langu hovyo halafu nitazame
Na waganga was kienyeji mbona wangenikoma
Wachawi wanaowanga mbona wangeisoma
[Verse 6]
Ningelia eeh, chozi lingenitoka
Maana tumerudia kama ya Sodoma
Naomba unisamehe ni mawazo tu
Nisikupangie wewe uliye juu
[PreChorus]
Maana mi mwenyewe sio mkamilifu
Ila huruma zako, zizidi tamalaki bwana
[Chorus]
Sijasema Bwana we ni kipofu
Ila naumia yamezidi maovu
Vipi ghadhabu yako we mwokovu
Ukija shuka nitaweka wapi sura Bwana
Aah aah aah ah (Mmh yelele mama)
Aah aah aah ah (Mmh yelele mama)
Yelele mama, yelele mama
Yelele mama, yelele mama
Yelele mama
Yelele mama
Yelele mama, yelele mama
Yelele mama
Written by: Obby Alpha

