積分

演出藝人
Zuchu
Zuchu
主唱
詞曲
Zuchu
Zuchu
詞曲創作
製作與工程團隊
Trone
Trone
製作人

歌詞

[Verse 1]
Nna hamu mwenzenu nna hamu kuyahadithia
Oh nna hamu tena nna hamu kuyasimulia
Utani kama utani tulianza kimasiara
Sikudhani, sikudhani yatafikia mahala
Akiwa hapatikani hapaliki sijalala
Kanifanya kitu gani mbona imekua mara
[Verse 2]
Dua la kuku menipata mwewe wallahi nyinyi ni mtihani
Hata makosa ayafanye yeye mimi ndo naomba samahani
[PreChorus]
Ona anacheka kama mazuri
Anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli
Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri
Na kwenye koma kaeka nukta kanitia na kufulii
[Chorus]
Baby mimi hapa taabani
Wewe utaniuwa-niuwa
Nimeoza dah yarabi sihemii
Wewe utaniuwa-niuwa
Izo raha zakoo
Wewe utaniuwa-niuwa
Roho yangu mali yako
Wewe utaniuwa-niuwa
[Verse 3]
Tukikosa stuli ni sunna kula kwenye mkeka
Unijue vizuri nikinuna mie ndo nadeka
Usijedhani kiburi uniache nikaja kuchekwa
Baby raha ya shughuli mkunwa awe na hekaheka
[Verse 4]
Husichokipenda wewe (Aah)
Chunga na mimi husinifanyie (Aah)
Mgomba wangu mwenyewe (Aah)
Eti ndizi nigombanie (Aah)
Nipe penzi nilewe niumbe nizimieumie
Ooh ringa kwangu upo mwenyewe kiboko yangu miee ooh vimbaa
[PreChorus]
Ona anacheka kama mazuri
Si anajua kabisa amenteka kwake sina shughuli
Eti kumwacha naanzaje sa kusepa natoa wapi jeuri
Na kwenye koma kaeka nukta kanitia na kufulii
[Chorus]
Baby mwenzako mimi twabani
Wewe utaniuwa-niuwa
Chagua mwenyewe unizike unishafirishe
Wewe utaniuwa-niuwa
Izo raha zakoo
Wewe utaniuwa-niuwa
Roho yangu mali yako
Wewe utaniuwa-niuwa
Written by: Zuchu, Zuhura Othman Soud
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...