積分
演出藝人
Rayvanny
聲樂
Diamond Platnumz
聲樂
詞曲
Diamond Platnumz
詞曲創作
Raymond Shaban Mwakyusa
作曲
製作與工程團隊
Diamond Platnumz
製作人
Aby Dady
製作人
Babydaddy
製作人
歌詞
Leo chereko-chereko, mwanenu nimekuwa
Zile kuringa mideko itapungua
Ahsante mama ulinifunza nkajua, baba kasema kuomba mwiko raha ya chumvi kununua
Tena si kwa nazi si hirizi za waganga, kwa baraka za baba na mama tu na dua
Waambie paparazi, pingamizi wenye viranga, waliosema hayawi hayawi yamekuwa
Iyena, Iyena, Iyena, Iyena
Iyena, Iyena, kwaheri tutaonana
Iyena, Iyena (Aah ooh), Iyena Iyena (Aah Iyeena), Iyena, Iyena, ntawakumbuka sana
Ndoa baraka, ukipata ushukuru, maana wanayoililia ni wengi sana
Kwetu talaka kuitoa ni kufuru, nimefunzwa vumilia niushinde ujana
Ili kesho mahususi kusudi wasinong'one, embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi nakuvisha waone, wakale sumu wavimbe wapasuke
Ati nashika nanga nteke nsichomoke ndani (Anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani (Anameremeta)
Sio vijembe vya kanga waziwazi mambo hadharani (Anameremeta)
Waliopanga mwenye nyumba kaja ndani (Anameremeta)
Iyena, Iyena (Aah iyoyo), Iyena Iyena (Aah Eeh), Iyena, Iyena, kwaheri tutaonana
(Kwaheri baba mama) Iyena, Iyena (Iyeena), Iyena Iyena (Aah Eeh), Iyena Iyena ntawakumbuka sana
Imefika tamati tulisubiri kitambo, leo samaki kanasa kwenye chambo
Pongezi kwa kamati yanavutia mapambo, napata picha safi, litanikoma bundle
Mwanamke usafi gaga kulisugua, mume akirudi shati, viatu kumvua
Kitandani marashi, massage kumchua, kisha anza sayansi viuno kutengua
Mambo ya kuzima taa si mahaba ni kuwanga, washa japo ka mshumaa, mumeo aone shanga
Makeup kinanda kaka suit kama mbunge (Anameremeta)
Mulo changa muda kujipooza na punje (Anameremeta)
Momo ndani Shivo amekuja na fumbwe (Anameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge (Anameremeta)
Iyena, Iyena (Aah iyee), Iyena, Iyena (Aah iyoyo), Iyena, Iyena kwaheri tutaonana
(Kwaheri baba mama) Iyena, Iyena (Iyee), Iyena, Iyena (Hhmm), Iyena, Iyena ntawakumbuka sana
Saa nataka kusasambua (Sasambu), me nasasambua (Sasambu), aby dad nasasambua mimi (Sasambu, sasambua tuone)
Mguu moja juu (Sasambu), usishushe chini (Sasambu), cheza jitazame (Sasambu, sasambua tuone)
Aisha kimobitel (Sasambu), nipe za baloteli (Sasambu), nyonga kibaiskeli (Sasambu, sasambua tuone)
Akaa kama unashika ukuta (Sasambu), ifanye unashusha (Sasambu), taratibu zungusha (Sasambu, sasambua tuone)
Sasambu, sasambu, sasambua tuone
Kama unawasha bajaji (Sasambu), imwagie na maji (Sasambu), tuwakomeshe vizazi (Sasambu, sasambua tuone)
Written by: Diamond Platnumz, Raymond Shaban Mwakyusa