積分

演出藝人
Rapcha
Rapcha
演出者
Vanillah
Vanillah
誦讀
Cosmas Paul Mfoy (Rapcha)
Cosmas Paul Mfoy (Rapcha)
饒舌
詞曲
Cosmas Paul Mfoy (Rapcha)
Cosmas Paul Mfoy (Rapcha)
詞曲創作
製作與工程團隊
Paul Peter Mnange (Papa)
Paul Peter Mnange (Papa)
製作人
David Juma Maganga (Yogo Beats)
David Juma Maganga (Yogo Beats)
混音師

歌詞

[Verse 1]
Someone is playing with me, kuna mtu ananichezea
Someone is playing with me
Nashuka kiuchumi ndoa yangu inachafuka
Kuna mchezo unaendelea they are playing with me
[Verse 2]
Muda mchache kwenye ndoa maumivu yamenizidia
Huu ni mwezi wa tano unaingia
Nkitazama muda ni saa sita usiku
Baada ya kumtafuta sana huyu mwenzangu ndo nyumbani anaingia
[Verse 3]
Niambie umetoka wapi Salma
Hii kesi isidingo si tumetoka kuisolve jana
Isingefika 40 missed calls ka ulikua kwa mama
Nakuambiaga huniheshimu Salma unanidharau sana, story zako mjini naambiwa
[Verse 4]
Hamna kitu kinaniuma kama habari kwamba mi namegewa
Unanipandisha hasira navokuambia ukweli
Afu unanijibu kwa kufoka kama unaonewa
Hebu Leta simu yako, fungua!
[Verse 5]
Salma usinipandishie, icho kiburi chako ntakupasua
Naichukua nianze kuipekua akaja kuikwapua
Akili ikaflip, gun nkanyanyua
[Verse 6]
Salma Kanijia juu, nimechoka maisha ya kubaniwa
Bora tu tuachane umezidi kunitishia
Story za malaya wako nikikuambia unajifanya mkali
Kama we kidume fyatua
Gun shots!
[Chorus]
Nilikupenda mpaka kufuru nikawa nawaza jidhuru ukiwa mbali
Tena nikakupa uhuru na ukashindwa shukuru ikawa ndo dosari
Ukaenda ku date na wale, mi wakuwa nasota we ule
Na mie kukuacha siwezi, ni bora dunia tuiache aah
[Verse 7]
Fahamu zinarudi akili imeduaa
Salma anateseka chini baada ya risasi nne kumvaa
Hofu kubwa inaniingia nikiangalia
Damu yake inavyonililia chini inatapakaa
[Verse 8]
Ndo Idea ya kukamatwa ikanijia
Nikajua haitopita muda mapolisi watanitimbia
Ila nguvu zote zishaniishia
Nikiumia kuona safari yetu ya mapenzi ilipokwamia
[Verse 9]
Dhambi inaanza kunitafuna
Natamani nirudishe muda nyuma niongee na Salma
Najiona mnafki kwa kumwaga damu kwa makosa ambayo moyoni najua kuwa na mimi nafanya
[Verse 10]
Itanitesa maisha yangu yote hii memory
Ego zetu zimefanya tumeharibu destiny
Vita na Insecurities hakukuwa na honesty
Na loyalty marafiki wakatunyima privacy
[Verse 11]
litimie agano
Nahisi Mungu ametuchagua mi na wewe tuwe mfano
Salma, hukustahili hii adhabu ninakiri
Naomba kabla haujafika mbali nisubiri
Gun shot!
[Verse 12]
Roho yangu inauma
Kosa lako kuzichezea hisia zangu
Inamaana hukuona
Nilivyopambana kuziheshimu hisia zako? Aah
[Chorus]
Nilikupenda mpaka kufuru nikawa nawaza jidhuru ukiwa mbali
Tena nikakupa uhuru na ukashindwa shukuru ikawa ndo dosari
Ukaenda ku date na wale, mi wakuwa nasota we ule
Na mie kukuacha siwezi, ni bora dunia tuiache aah
Written by: Cosmas Paul Mfoy (Rapcha)
instagramSharePathic_arrow_out

Loading...