Lyrics

It's Bonga (Oh nah nah nah nah nah aah) Asante Mungu Baba uliye mwema Nimeiona siku nyingine ya furaha Hali sio haba sio njema Wa kuniponya nipate hata chembe ya furaha Maana wazazi wananitegemea Na ninakaribia mi kuitwa Baba Nami ndunguzo waloegemea Sina kitu nimechalala nimevava Uniepushe mabaya dunia Yasijenikumba Napiga goti kwa uchungu nalia Ni nusuru muumba Katu nisikate tamaa Niende kusaka tonge Nipate ama nishinde njaa Moyoni upige konde, ni sawa eh! Ni sawa, ni sawa Nami nitafika (Ata nikikosa sawa) Ni sawa, ni sawa Nami mimi utanipa (Ah ridhiki we ndo unayegawa) Sawa, ni sawa Nami nitafika (Mwanadamu hawezi panga) Ni sawa, ni sawa Nami mimi utanipa (Sitozuguka kwa waganga) Natapa tapa elimu sina Mi kusoma sijasoma Nami nasaka nijenge heshima Mi nakoma ju wananichoma Ni wewe pekee ndo naye jua Ah mbele yangu na nyuma yangu Mie mpweke naomba dua Ah Baba fungua ridhiki zangu Nashukuru Baba, pumzi unayonipa Maisha naendelea Ila kingine Baba, nadhalilika Huu mzigo unanielemea Baba niwewe Baba (Ni wewe) Niwe ndo msaada (Ni wewe) Ni wewe, ni wewe Baba ni wewe Uniepushe mabaya dunia Yasijenikumba Napiga goti kwa uchungu nalia Ni nusuru muumba Katu sikate tamaa Niende kusaka tonge Nipate ama nishinde njaa Moyoni upige konde Ni sawa, ni sawa Nami nitafika (Ata nikikosa sawa) Ni sawa, ni sawa Nami mimi utanipa (Ah ridhiki we ndo unayegawa) Sawa, ni sawa Nami nitafika (Mwanadamu hawezi panga) Ni sawa, ni sawa Nami mimi utanipa (Sitozuguka kwa waganga)
Writer(s): Ibrahim Nampunga Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out