Lyrics

(Mwamba La Mombala) Wengine wananipenda, baadhi wananipoda Wengine wananisifia, eee, wengine wananipondea Sitoweza kuwatenga, sitoweza kuwatenga Hata kama wakiponda daima nitawapenda Wanaona nawabana, maovu wanayafanya Hali hii itakuwaje mi' nitapoiaga dunia Wengi watalia, wengine watafurahia Siku itakapofikia utapoiaga dunia Wengi watalia, wengine watafurahia Siku itakapofikia mi' nitapoiaga dunia Wali kufa-kufa nawengine kifo wananiombea Wali kufa-kufa nawengine kifo wanakuombea Nikifikiria kifo, kulala siwezi siitaji mpenzi na sifanyi ushenzi Naitaji nikae tu, nimuombe mwenyezi Siku ya kifo changu anipemema makazi (Ukimaliza kuteseka unakwenda kule) (Hileee ndio nyumba ya milele) (Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele) (Ukimaliza kuteseka unakwenda kule) (Hileee ndio nyumba ya milele) (Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele) Maisha ni kutoka, kisha kuchakaa Yani ukishafika juu nikudondoka Umepita kwenye raha, shida ni balaa! Pumzi imeshakata ndio unapanda moto car Mpende mama mtenge baba ndicho umejenga The way uta'cholipwa ndicho umetenda Tuko up, tuko down, muda unakwenda Tupo njia ya Kanumba na Papa Wemba Dada, Mama, Baba m'nanitenga zikifika nitaondoka bila kupenda Unapojenga ukipenda funga lanter nitazima kamshuma, kisha nakuenda Naona kuna dondo kapigwa panga Chini hakuna godoro kuna michanga Mida yakula moto kufunga kanga Sasa regeza kidogo, kaza kamba Sitaki tena mbido nataka mwanga Upepo sina majo sina nipe sanda (Ukimaliza kuteseka unakwenda kule) (Ileee ndio nyumba ya milele) (Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele) (Ukimaliza kuteseka unakwenda kule) (Hileee ndio nyumba ya milele) (Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele)
Writer(s): Abbas 20 Percent Hamis, Abbas Hamis, Issa Rorexxie Ibungu, Issai Ibungu Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out