Texty

Dear boys dear... men Ni sisi wasichana kina dada, mabinti na mama zenu Tunaongea kutoka upande wa chini, upande mbali upande kutoka usawa wenu Upande nilipo msichana kuna hitilafu 'So' sikio lako thabiti ni ushindi kwangu Ninayotaka kusema hapa sio siri katu Ili ujue nina vingi vya ku-offer kabla ya mwili wangu Kwa miaka mingi nimeishi gizani Gizani kwenye baridi na miba mingi nyikani Eneo uliotaka niishi ni eneo kandamizi Na bahati mbaya we' ndo' mchoraji wa hii ramani Ramani inamwonyesha binti kama chombo cha mapenzi Msindikizaji mtoto tegemezi Ramani isiyojua vituo Isiyojua tunaweza kuwa marafiki bila kuvuana nguo Dear boys, dear men Mngeelewa mngeiweka fikra sahihi Kama sanaa jinsi inavyozalisha fasihi Mi' ni mlezi ukinivika mi' umeivika jamii U-gentlemen sio kulipa mgahawani Umeshapitwa na wakati Hainisaidii kunifungulia mlango nikifika kwenye gari Nifungulie fikra nitafakari Dear boys, dear men Tumekuwa tegemezi maana mmeficha mbegu Nani wa kuipigana vita yetu Umbali kati yetu utakuwa mkubwa milele Maana si ni wahanga wa mifumo mliyoiunda wenyewe Nikijaribu kusoma nabaki bure Maana unajali mwili wangu, ndo' maana sitaki shule Kila nikienda popote wanaomba ngono Labda niwe changudoa to the fullest At least I'll get paid Hata sisi tuna life too And the world doesn't revolve around you Nipo tofauti sikupenda, na tena Unaponichezea fahamu kuwa ninazeeka mapema Shujaa unakumbukwa mzazi sikumbukwi Na kwanini kuwa msafi sio haja kwako Au kutembea kifua wazi ni kujiamini Nikitembea mimi ni nusu uchi I wish ungejua pride yako nayo sumu I wish ungejua kuwa uanaume sio nguvu I wish ungejua kuwa binadamu hajakamilika Mwanaume aliyekamilika anatimiza majukumu I wish ungejua kuwa na mimba sio haya I wish ungejua mwanamke kuwa kichwa si vibaya I wish ungejua kuwa upendo nao una nguvu kwahiyo mwanamke akitongoza Mwanaume si malaya I wish ungejua kuonyesha fear sometimes, it's okay It's okay kulia sometimes I wish ungejua uongozi hauoni jinsia si Tatizo mwanamke kuongoza njia sometimes Mifumo mliyoianzisha ina maisha Na chenye maisha kinazikwa Kwahiyo ipo siku mwanamke atasimama Na vita tunayopigana tutashinda Inasikitisha hamkui kihisia, japo mnakua kiakili Natamani... natamani mngejua kuwa inauma sana kuwa namba mbili kwenye kila nyanja Ego ni power ila iogope Maana ni upanga unaokata pande zote Ngoma nzuri ngoma nzuri haitavuma milele Ukitumia ubabe vibaya utakuvunja mwenyewe Hadithi ya mwanamke alimshawishi Adam kula tunda Iliandikwa na wewe Sijui Delilah alichukua nguvu za mumewe akaziuza Iliandikwa na wewe Upande wangu wa hadithi haujasikilizwa Pengine hautasikilizwa hasirani Maana ulianzisha shule akasoma mwanaume Mwanamke nikabaki nyumbani Dear boys, dear men Hamtakaa kwenye kilele Maana kilele ni kuwa mama Mi' ni kichwa sio wewe ungekuwa kichwa Mtaani kusingekuwa na single mothers Lini mtaacha kutuita mademu Au labda mwite demu mama'ako Ukiona hauwezi naomba niheshimu kwa maana heshima inaanza kwako Na haja ya maelewano iko hapo I mean... ipi salama ya kichwa cha familia bila Mkono wa kuosha macho? Najua tupo tofauti Na tofauti yetu itabaki, itabakia hivyo milele Ila naomba usinichukie nielewe Dear boys, dear men Ni sisi wasichana, kina dada, mabinti na mama zenu Tunawasilisha kutoka upande wa chini upande wa pili Upande mbali kutoka usawa wenu Dear girls, dear Women Ni sisi kina kaka, kina baba, wanaume machizi wenu Tunaongea kutoka upande wa juu, upande wa mbali Upande uliowekwa na asili yetu Upande wenye mafungu yenye ulanguzi Upande wenye uthubutu na maamuzi Upande wenye machozi jasho na damu Uongozi upako ufahamu, upande usio na uhuru na uchaguzi Upande uliofanya wanaume tutengwe na tunu Tutengwe na tunu Upande ambao pengine kuishi wewe ni ngumu Upande ambao asali yake ni kilele cha sumu Upande ambao haushabikii tija ya upendo au furaha au amani Kama hauangalii pima utagundua upande niliosimama mimi ni ngao ya jamii nzima Uanaume sio ushindi ni jukumu Uanaume sio rizki ni hukumu Ungejua kwanini wanaume wana msongo wa mawazo pengine ungefurahia udogo wako Dear women, dear girls Mmekuwa chombo cha ngono Maana mmetufanya chombo cha fedha Kama nguo hazitabadili mishono Hatuwezi kuwa marafiki bila ngono nawaeleza Mnapoona padogo pana taswira ndefu Kiasi haujui si ndio tuliopigana vita yenu Hata mkiamka mmekuwa wanaume leo Mtagundua kuwa jinsia sio cheo Wapendwa tukishindana mtashindwa Hata mkishinda ushindi wenu hautalindwa Kama ambavyo kila mmoja anatumia choo chake Kila mmoja a-play role yake na awe bingwa Dear women Ndoa sio mafanikio Kuna wengi wanakonda maana ndoa zao sio Ndoa ni mwiba usijivune Ukiipata niamini unaweza kukamilika bila mume Dada baki shule bila elimu utateseka Ukitegemea urembo ipo siku utazeeka Kama ukiweka mwili wako hisani Ukizeeka tutajali ulichonacho kichwani 'Skiza' hata wanaume tuna doubts too And this world doesn't revolve around you Tuna stress zinatufunga na tena Kazi zetu ni ngumu ndo' maana tunakufa mapema Kama unahisi upo huru umepotoka Hauwezi kuwa huru wakati umelipiwa posa Dear women It's okay kuwa namba mbili Majukumu sio mashindano acha kukalili It's okay kumlea mwanaume asiye na kazi Ukaendelea kumuheshimu bila kumshusha hadhi Mbona sisi tunalea wanawake masikini wamekata ringi na bado mtaani hatutatangazi Mwanaume ana jukumu la kujenga msingi? No, msingi unajengwa na elimu Kwa mfano nani anayekubali kucheza uchi kwenye videos? Jiheshimu nikuheshimu Urembo pia ni power, ila ni power na iogope Maana ni upanga unaokata pande zote Ngoma ya uzuri haitovuma milele Ukiutumia urembo vibaya utakuvunja mwenyewe I wish ungejua unachowaza ni muhimu Ukifanyia kazi na kuwa wa kwanza si' majibu I wish ungejua kwamba asili imenipa umwamba Nikulee, kukulea wewe ni msaada si' wajibu I wish ungejua tuko tofauti hata utunge dini Hauwi mwamba kwa kumweka mwanaume chini I wish ungejua kuwa kichwa ni hukumu Maana hakuna kinachotisha kama jukumu Wangapi tumelelewa na hao single mothers Maskini and we turned out just fine Maybe idea ya kuacha kujali mtoto sababu Baba mjinga ingeachwa far behind Tunasubiria uhalisi ubadilike Labda uhalisia haubadiliki huu Labda ni wakati wa kukubali ili yaishe kwamba Mtoto ni wa mama na baba ni rafiki tu Lini mtaacha kutuita madanga ma-sponsors? Ndio, niheshimu nikuheshimu nitaacha wewe Ukiona imetosha, au sio? Najua tuko tofauti Na tofauti itabaki hivyo milele Usinichukie nielewe Dear girls, dear women Ni sisi kina kaka kina baba, wanaume machizi wenu Tunawasilisha kutoka upande wa juu, upande mbali uliowekwa na asili yetu
Writer(s): Edger Mwaipeta Lyrics powered by www.musixmatch.com
instagramSharePathic_arrow_out